Wafalme Huota Nini

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Wafalme Huota Nini
Loading
/
Danieli 2:36-45

Hujambo na karibu.

JE WAFALME HUOTA NDOTO ZA AINA GANI?

Ndilo tunajaribu kujibu leo, tukiongozwa na Neno kutoka kitabu cha Danieli 2:36-45.

Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Karibu tujifunze Neno katika kipindi hiki cha ‘Matumaini’

Leo twalichambua Neno la Mungu kutoka kitabu cha Danieli 2:36-42 (x2)

Nasoma:

36 ‘Hii ndiyo ile ndoto nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme.

37 Wewe Ee Mfalme, U mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa Ufalme na uwezo na nguvu na utukufu.

38 Na kila mahali wakaapo wanadamu, Wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote, wewe U kichwa kile cha dhahabu.

39 Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe, na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.

40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma, kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda na kama chuma kisetavyo (crushes) vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunjavunja na kuseta.

41 Na kama ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi na nusu chuma , ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.

42 Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakaokuwa nusu yake una nguvu na nusu yake umevunjika.

43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu lakini hawatashikamana kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.

44 Na katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake, bali utavunja falme hizi zote vipande na kuziharibu nao utasimama milele na milele.

45 Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono na yakuwa lilivunjavunja kile chuma na ile shaba na ule udongo na ile fedha, na ile dhahabu, basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye na ndoto hii ni ya hakika na tafsiri yake ni thabiti.’

Ndoto, ni jambo la kawaida, lakini la kushangaza ni vile Mungu alivyomnunulia mfalme aliyemcha Mungu, historia na ndoto hiyo twapata kweli za Maisha yote. Mfalme aliota ndoto lakini akasahau, lakini kwa uweza wake Mungu, Danieli aliweza kumkumbusha ile ndoto na kumpa tafsiri. Tafsiri yake Danieli itahusu dunia yote.

  1. Kichwa cha dhahabu, kilionyesha ni ufalme wa Babiloni.
  2. Kifua na mikono ya fedha – ufalme wa Pashia na Media
  3. Tumbo na viuno vya shaba – Ufalme wa Ugiriki.
  4. Miguu yake ni chuma- Ufalme wa Kirumi, haupo sasa lakini utafunuliwa tena miaka ijayo.
  5. Nyayo za miguu yake nusu chuma na nusu ya udongo – mataifa yanayounga muungano wa mataifa ya Ulaya.

Na katika mstari wa 44 kitabu cha Danieli 2:44 twapata maneno haya:

‘Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele wala watu wengine hawataachiwa enzi yake, bali atavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu nao utasimama milele na milele’

Halafu maneno ya mstari wa 45.

‘Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, nayakuwa lilivunjavunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo na ile fedha na ile dhahabu, basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye, na ndoto hii ni ya hakika na tafsiri yake ni thabiti.

Ndoto hii ni hakika na tafsiri yake ni thabiti.

Mambo kwisha!!

Baada ya hayo, Mungu ataifunga historia, na mfalme Yesu Kristo, Mfalme wa Wafalme, siku moja atarejea mahali pake katika ufalme wake. Mungu mwenyewe atauweka na kuuleta ufalme huo kwa wakati wake, unaofaa.

Je, wewe utakuwa mmoja wa watakaouridhi ufalme wa Bwana Yesu?

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!