Utukufu Katika Bwana

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Utukufu Katika Bwana
/
1 Wakorintho 1:1-9

Hujambo na karibu leo katika ‘Matumaini’. Twalichambua neno la Mungu kutoka 1 wakr 1:1-9, ‘utukufu katika Bwana’

Jina langu ni David Mungai, karibu. Wimbo kwanza halafu tuendelee.

WIMBO

Karibu tena tujifunze Neno 1 wakr 1:1-9

Mji wa Korintho, kama ilivyo kawaida, ulikuwa na shughuli nyingi za kibiashara.

Acropolis, ni mahali palipo inuka mjini kote na ndipo palikuwa na ofisi nyingi za kiserikali, na ndipo palipokuwa pamejengwa hekalu ya mungu wa kike Aphrodite, na ulikuwa na makahaba 1000. Wakorintho waliabudu unajisi.

Hata hivyo, mjini Atheni kulikuwa na wasomi wengi -hasa wasomi wa philosophia. Imerekodiwa vizuri sana wakati Paulo alitembea Korintho pale mlimani wa Mars alijaribu kuwarekebisha.

Mwaka mmoja na nusu, Paulo alikuwa Korintho akijaribu kuwasaidia wakorintho kumjua Yesu Kristo na kukua kiroho. Paulo, alitamani sana, kuona na kusikia kanisa la Korintho lina sifa njema. Pamoja na hayo, Paulo alifanya kazi ya kutengeneza hema akiwa pamoja Akwila na Priscilla.

Aliongea sana na wayahudi katika sinagogi yao. Na kwa sababu wayahudi walikuwa na vichwa ngumu, Paulo alienda kukaa katika nyumba ya Yustu, amabaye nyumba yake ilishikana na sinagogi. Kanisa la Korintho halikuwa na msingi imara, lakini Paulo alitamani sana kuwasaidia wakristo kukua na kuimarika kiroho.

Nasoma sasa, fungu hili la neno, 1 wakr 1:1-9

1 Paulo aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene NDUGU YETU,

2 Kwa kanisa la Mungu lililOKO Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana Yesu Kristo, kila mahali, Bwana wao na wetu.

3 neema na iwe kwenu na Amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo

4 Namshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu niliyopewa katika Kristo Yesu

5 Kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote

6 Kama ushuhuda wa Kristo uliyodhibitika kwenu,

7 Hata hamkupungukiwa na karama yoyote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo

8 Ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo

9 Mungu ni mwaminifu amabaye mliitwa na yeye mwingune katika ushirika wa mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu

Kutoka kwa fungu hili la neno, twapata kweli tatu muhimu zinazotuhusu sisi tunaomwamini Yesu na uhusiano wetu na Bwana

 1. mst 2 Wanaomwamini Yesu wametakaswa. Tumetakaswa kwa sababu tumemwamini Yesu Kristo. Yaani, tumetengwa, tumebadilishwa mwendo, n ahata ushirika wetu na watu wengine mtu anapomwamini Yesu Kristo, Mungu humfanya yule mtu kuwa kiumbe kipya
  Ingawa yule mtu bado yupo duniani hii, nia na malengo yake hutamani kumtukuza Mungu kwa maneno na vitendo, kabla ya kumwamini Yesu mtu humtumikia yule mwovu shetani, lakini baada ya kumwamini Yesu, mwenyezi Mungu hutuumba upya mioyoni na akilini. Tumetakaswa katika Kristo
 2. katika mstari wa 5, twaona ya kwamba, tumetajirishwa katika Kristo.
  ‘Kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye katika maneno yote’
  Na katika warumi 5:20, Paulo aueleza ukweli huu kwa maneno haya.
  ‘Lakini sharia iliingia, ili kosa lile liwe kubwa sana na dhambi ilipozidi neema ilikuwa nyingi zaidi’
  Twaokolewa kwa neema, haijalishi ukubwa na uovu wa dhambi neema ya Mungu ina uwezo wa kuondoa dhambi yote. Kwa Imani, ila si kwa matendo.
  Neema ya Mungu imetufanya matajiri wa ondoleo la dhambi zetu na kwa Imani twajitawalia wokovu ulivyo mkuu.
 3. Tunao utajiri kwa sababu ya ushirika wetu na Yesu Kristo. Nasoma mstari wa9 ‘Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingine katika ushirika wa mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu’
  Ni vyema na muhimu, kumshukuru na kumtukuza Mungu, kwa ushirika tulio nao katika Yesu Kristo. Kumbuka ya kwamba, licha ya matatizo duniani hii, uhusiano wetu na wa Yesu ni milele. YESU KRISTO ASEMA, ‘Na sasa, Baba unitukuze mimi, pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuweko’
  Uhusiano wetu na wa Yesy -Immanueli ni Mungu pamoja nasi milele na milele.
  Mkristo ni Tajiri katika Kristo
  A) Katika kristu tumetakaswa
  B) Katika kristu tu matajiri wa Imani
  C) Katika kristu tuna uhusiano na Mungu -daima na milele na milele tu watoto wake. Ni yeye hutuimarisha katika Imani.