Usiwategemee Watu – part 2

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Usiwategemee Watu – part 2
/
Mwanzo 4:9-12

Ni wakati wa kulichambua neno la Mungu katika kipindi hiki cha matumaini. Somo letu lapatikana kutoka mwanzo 4:9-12. Jina langu ni David Mungai. Msikilizaji kila mmoja wetu anao cheche ya wema ndani yake, na ikipepetewa huwa miali ya moto. Lakini twaona ya kwamba mambo huwa kinyume na ukweli huo. Badala yake chuki na dharao zimejaa mioyo yetu. Kwa nini? Kwa sababu hali ya mioyo yetu huwa hivyo. Historia imeonyesha hivyo. Nasoma kutoka Mwanzo 4:9-12


“Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako? Akasema sijui mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Akasema umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa umelaaniwa wewe katika ardhi iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako. Utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake, utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.”


Hapa twapata mazungumzo kati ya Mungu na kaini. Kaini aulizwa na Mungu kama amemwona Habili ndugu yake. Tayari alikuwa amemuua, na hapa anasema kwamba hajui alipo, lakini alijua kwa sababu alikuwa amemwua. Baada ya dhambi ya kuua sasa afuatisha dhambi ya udanganyifu. Ukitenda dhambi moja itakuelekeza kwa nyingine. Kaini alikosea kufikiri kwamba angeficha dhambi Mungu asijue. “Sijui mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”

Habili akawa mkaidi kwake Mungu. “Mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” ni kama kumwuliza Mungu, kwani ulinipa kazi hiyo? Ukijaribu kufunika dhambi ni ukaidi wa hali ya juu, maana tayari Mungu akujua na anayosoma hata hisia na mawazo yako. Heri ukitenda dhambi, utubu pale pale kuliko kuificha maana katika hali ya kuificha utatenda dhambi Zaidi. Mungu alimuuliza kaini umefanya nini? Kwa sababu. “Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi..umefanya nini? Kwa hiyo, sasa umelaaniwa wewe katika ardhi iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako, utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake, utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.” Maneno hayo hayo nyoka aliambiwa “Kwa sababu umeyafanya hayo (kumdanganya Hawa) umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni, kwa tumbo utakwenda na mavumbi utakula siku zote za maisha yako.”

Kaini awekwa kundi moja nyoka, muasi na mkaidi na mwenye hila na chuki muuaji. Mungu akauondaa msaada wake kwa kaini wa kila siku. Kaini akawa hana kwake duniani. Sote kama kaini tumetenda dhambi. Mungu ampenda mwenye dhambi lakini aidharau dhambi. Dawa ya dhambi ni kumwapmini Yesu Kristo, naye atakusafisha na damu yake aliyoimwaga pale msalabani. Kwa huruma zake Mungu hutusamehe nakuziondoa dhambi zote, tukitubu na kuungama dhambi zetu. Yeye ni mwingi huruma na upendo. Mwamini Yesu.