Ushindi Ni Wetu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Ushindi Ni Wetu
Loading
/
I Wakorintho 9:19-27

Hujambo na Karibu tujifunze Neno pamoja. 1 Wakorintho 9:9-27 “USHINDI NI WETU” Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo halafu tuendelee

Wimbo

Naam. Karibu tena tujifunze Neno pamoja. Tunapookolewa kwa kumwamini Yesu ni tarajio lake Yesu maana katika Injili ya Marko 16:15, Asema; “Enendeni ulimwengu mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” kwa nini? Jibu lapatikana katika Injili ya Yohana 3:16 “kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ila kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.”

Sasa tusome fungu letu la leo. 1 Wakorintho 9:19-27

19 Maana ingawa nimekuwa huru kwa watu wote nalijifanya mtumwa wa wote, mpate watu wengi zaidi.

20 Nalikuwa Kama myahudi ili niwapate wayahudi, Kwa wale walio chini ya sheria (ingawa mwenyewe si chini ya sheria). Ili niwapate walio chini ya sheria.

21 Kwa wale wasio na sheria, nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo, Ili niwapate hao wasio na sheria.

22 Kwa wanyongenilikuwa mnyonge. Nimekuwa hali zote nipate kuwaokoa watu.

23 Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili Ili kuishiriki pamoja na wengine.

24 Je! Hamjui ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, Lakini apokoaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.

25 na kila ashindanaye katika yote, basi hao hufanya hivyo. Kusudi wapokee taji isiyoharibika.

26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asifaye, napigana ngumi, vivyo hivyo, si kama apigaye hewa.

27 Bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha, isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wakukataliwa.

Katika harakati zetu za kuhubiri, ni vizuri na vyema, kuhakikisha ya kwamba tumefikisha kiwango cha kufamanika. Tujitoe kuwa watumishi wanyenyekevu kwa wote. Paulo alijitoa kwa wayahudi na watu wa mataifa kwa waliokuwa huru, maskini na matajiri.

Paulo aliwapa kielelezo cha mashindano ya isthmiah, yaliyofanywa Karibu na mji wa korintho, kila miaka miwili ndipo akawaambia, mst 25. “Na kila ashindanaye katika mchezo hujizuiya katika yote, basi hao hufanya hivyo, kusudi wapokee taji iharibikayo, bali sisi tupokee taji isiyoharibika.”

26-27. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo si kama apigaye hewa. 27. Bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Paulo ahofia kuhubiri na kutumika kwa bidii na akawa mmoja wa wale ambao hawatapata taji ya utumishi bora kama tunavyosoma katika 1 Wakorintho 3:13-15.

13 Maana siku ile itaidhihirisha kwa kuwa yafunuliwa katika moto, na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.

14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.

15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa, Lakini ni kama kwa moto.

Na katika Yohana wa pili mstari wa 8. Waraka wa pili wa Yohana wa pili una sura moja tu. Nasoma mstari wa nane” Jiangalieni nafsi zenu, msiyapoteze mliyoyatenda bali mpokee thawabu timilifu.” Mst 26 mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama apigaye hewa, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha, isiwe nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe wa kukataliwa.”

Yaani Paulo atuonyesha kuwa katika huduma ya kuhubiri Injili lazima tuwe na nidhamu- tunayoyasema tuyadhihirishe kwa vitendo, bila ulafi.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!