Umoja Wa Mwili Wa Kristo

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Umoja Wa Mwili Wa Kristo
Loading
/
I Wakorintho 12:12-26

Hujambo na Karibu tujifunze Neno pamoja. 1 Wakorintho 12:12-26

“UMOJA WA MWILI WA KRISTO” Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo halafu tuendelee

Natumai u buheri wa afya, na ni furaha yetu kukukaribisha, tujifunze neno pamoja, katika. 1 Wakorintho 12:12-26, umoja wa mwili wa kristo.

12 maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo

13 kwa maana katika Roho Mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu wayahudi au kwamba tu wayunani, ikiwa tu watumwa au ikiwa tu hivi nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja

14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali li vingi

15 Mguu ukisema, kwa kuwa mimi si mkono mimi si wa mwili, je, si wa mwili kwa sababu hiyo?

16 Na sikio likisema kwa kuwa mimi, si jicho, mimi si la mwili. Je, si la mwili kwa sababu hiyo?

17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?

18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka

19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

20 Lakini sasa viungo ni vingi , ila mwili ni mmoja

21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, sina haja na wewe, wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja na ninyi

22 Bali Zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge Zaidi vyahitajiwa Zaidi

23 Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima Zaidi, na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri Zaidi sana

24 Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji, bali Mungu ameuunganisha mwili na kukipa heshima Zaidi kile kiungo kilichopungukiwa

25 Ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vifunzane kila kiungo na mwenziwe

26 Na kiungo kimoja kikiumia viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa viungo, vyote hufurahi pamoja nacho

Katika neno hili la Mungu, Paulo anatuonyesha umuhimu wa uhusiano mwema kwa kila mmoja wetu katika mwili wa Kristo -kanisa kama vile tumesoma kutoka mistari ya 12-13, Roho Mtakatifu wa Mungu ametuunganisha katika mwili mmoja, mkubwa kwa mdogo. Baadhi yet utu wadogo lakini kama viungo dhaifu vilivyo muhimu ndivyo tulivyo, viungo hivyo vikiumia , mwili wote huumia. Viungo vyote hufanya kazi pamoja, tena kwa heshima na kila kiungo hutunza mwenza

Swali ni hili, tumeunganishwa namna gani? Mst 13. kwa maana katika Roho Mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu wayahudi au kwamba tu wayunani, ikiwa tu watumwa au ikiwa tu hivi nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja

Daima tu viungo vya mwili wa Kristo. Na kama vile viungo huvalishwa heshima kila kimoja humpa heshima mwili wote. Sisi pia kila mmoja wetu, vile tunavyoonekana wenye hekima, ndivyo na mwili wote (kanisa) heshima zako ni zangu na kanisa lote kwa utukufu wa kichwa YESU milele na milele.

Na katika mistari 21-26 twaoona ya kwamba, huu mwili,kanisa wengi wetu hawaonekani, lakini tu wa maana sana kwa sababu, twapiga vita vyetu kwa magoti yetu huwaombea viungo vingine vyote, haya ni kwa mapenzi yake bwana, wetu wetu Yesu Kristo

Tumtimikie popote tulipo kuwahudumia ndugu na dada katika Kristo haijalishi rangi au hali ya kimaisha

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!