Uhakika Wa Neno

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Uhakika Wa Neno
Loading
/
Yohana 6:13

Msikilizaji, natumai u buheri wa afya. Naitwa David Mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi hiki cha Matumaini.

Leo twalitazama neno kutoka aya mbalimbali kuhusu kusaidika kwa Neno. Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO


Naam karibu tena. Je, twawezaje kulisadiki neno la Mungu ndilo swali twauliza katika Matumaini leo.

Yesu alisema: injili ya Yohana 6:63

“Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena na uzima.

Tunaweza kulisadiki neno kwa sababu Yesu mwenyewe alisema ya kwamba, Neno lake ni uzima. Na katika injili ya Yohana 5:39 Yesu alisema.

“Mwayachunguza maandiko kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake na hayo ndiyo yanayonishudia.”

Twalisadiki neno la Mungu- Bibilia, kwa sababu linamshuhudia Bwana wetu Yesu Kristo; ukitamani kuyajua mengi yanayomhusu Yesu Kristo, mwokozi na mkombozi wetu. Lisome na ulitafakari neno la Mungu.

Katika injili ya Yohana 14:24 twapata maneno haya. Yesu alisema:

“Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia sio langu ila ni lake Baba aliyenipeleka.”

Tunaweza kulisadiki neno la Mungu kwa sababu ni neno la Mungu, muumba wetu na muumba wa mbingu na nchi. Na hii ndiyo sababu twasema katika injili ya 1:37 twasoma.

“Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.”

Malaika wa Bwana alitumwa na Mungu, kumwambia Elisabati, ingawa alikuwa tasa; Mungu alimwezesha Elisabati kujifungua motto; jina lake Yohana, aliyekuwa mpatizaji. Pamoja na haya, Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu, akamwambia ingawa alikuwa bikira atajifungua motto Yesu.

Ni ikawa hivyo, Mariamu akiwa angali bikira Mungu kwa uwezo wake akamfanyia muujiza Mariamu – bikira akajifungua motto Yesu. Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Unaweza kulisadiki neno lake Mungu.

Tunaweza kulisadiki neno la Mungu, kwa sababu ni mawasiliano yetu na Mungu. Ni mawasliano maalum. Neno la Mungu – Bibilia liliandikwa na waandishi takriban arobaini, ikachukua muda wa miaka 1500 – Bibilia yote ni vitabu 66 – 39 katika Agano la Kale na 27 katika Agano jipya, na vitabu vyote havitofautiani. Kwa akili zetu, hiyo haiwezekani, lakini kwa nguvu, na uwezo wa Roho Mtakatifu hayo yawezekana.

Neno la Mungu ni kamili na ni la kusadikika. Katika waraka kwa Waebrania twapata maneno haya. Waeb 1:1-2 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika, aliyemweka kuwa mrithi wa yote na tena aliufanya ulimwengu.

Yesu akawa mawasiliano ya upendo kutoka kwa Mungu nasi tukauona na kuupokea ushuhuda huu kwa kumwamini na kumpokea Yesu mioyoni mwetu. Neno la Mungu lasemwa; Neno la Mungu ni sauti yake Mungu. Kwa hivyo laweza kusadikika. Na ni mawasiliano yake Mungu.

Yesu alilikariri neno wakati wa majaribu – alipojaribiwa na Yesu Kristo. Akamshinda shetani. Neno la Mungu ni la kusadikika na kuaminika kwa sababu lina nguvu na uwezo wa ushindi.

Neno la Mungu – Bibilia ni la kusadikika.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!