Twapaswa Kumwamoni Mungu Wa Biblia

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Twapaswa Kumwamoni Mungu Wa Biblia
/
Isaya 26:1-9

Hujambo msikilizaji wangu. Kwaribu tujifunze neon pamoja. Twalichambua fungu la neon kutoka chuo cha nabii Isaya 26:1-9, twa paswa kumwamini Mungu wa biblia. Jina langu ni David Mungai, kbala ya hayo yote, wimbo kwanza.

Naam karibu tena msikilizaji. Kuna Dini nyingi sana duniani na dini zote binadamu ndiye hamtafri Mungu lakini katika ukristo, Mungu ndiye humtafuta binadamu ili amwokoe na janga la dhambi hii ndiyo sababu Yuesu Kristo alishuka kutoka Mbinguni mpaka Duniani kusudi tupate njia ya wokovu kwa kutubu dhambi zetu na kumpokea mwokozi Yesu moyoni na maishani mwetu.

Biblia husema na kutangaza Mungu wa Kweli katika Yesu Kristo. Hii ndiyo sababu mungu asema nasi kwa maneno haya, ‘sikiza eeh Israeli, mwana mungu wetu, bwana ndiye mmoja, 5 nawe mpende bwana mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu yako yote, Kumbukumbu la Torati 6:4-5

Swali; kwanini tumwamini mungutunayemsoma katakana ndani ya biblia-neno la mungu-? Jibu twalipata katika chuo cha nabii Isaya 26:1-9

1 Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.

2 Wekeni wazi malango yake, Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.

3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.

5 Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, Mji ule ulioinuka, aushusha, Aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini.

6 Mguu utaukanyaga chini, Naam, miguu yao walio maskini, Na hatua zao walio wahitaji.

7 Njia yake mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.

8 Naam, katika njia ya hukumu zako Sisi tumekungoja, Ee Bwana; Shauku ya nafsi zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako.

9 Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.

Jibu; kwa sababu Mungu wa biblia Ndiye ukweli na ukweli ndio chanzo cha hekima. Pamoja na hayo, nabii isaya asema kwamba kwake mungu tapata haki na amani.

2 Wekeni wazi malango yake, Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.

3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini

Taifa la haki hushika ukweli.

Sote na tusikia katika taifa hili. Taifa lenye haki husikia ukweli. Na mungu wetu katika Kristo Yesu ndiye kweli. Ukiwa na Mungu moyoni, na ndiye kweli na haki, atajidhihirisha. Musa aliyekiandika kitabu cha kumbukumbu la torati amesema hivi katika sura ya 32:4 yeye mwamba, kazi yake ni kamilifu maana njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, yeye ndiye mwenye haki na adili kwa hiyo, twapaswa na ni muhimu kumwamini mungu na biblia.

Pamoja na hayo, ni mungu wa haki na wa kutegemewa neon lasema,

3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini

Mtume daudi, katika zaburi 18atatia mkazo ukweli huukwa kwa maneno haya

1 wewe bwan nguvu zangu nakupenda sana, bwana ni Jabali lagu na boma langu na mwokozi wangu mwamba wangu, mnayekimbilia ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.

Na katika na kwa jina lake, mungu, linao ushindi maana ufalme wake upo ndani ya kila anayemwamini Yesu kristo. Ufalme wake umo ndani yetu kwa yeyote amwaminiaye Yesu kristo.

Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutemea. Huyu dniye mungu wangu wa kuaminika ndiye mwamba wa mbingu na nchi.