Tumia Akili Vizuri Utafanikiwa

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Tumia Akili Vizuri Utafanikiwa
Loading
/
Mwanzo 41:25-45

Hujambo na karibu. Naitwa David Mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi hiki cha matumaini. Twalichambua neon kutoka Mwanzo 41:25-44. Namna ya kutumia akili-unufaike.

Labda umejaribu mambo mengi bila kufanikiwa. Lakini ukitamani na kupenda kuwa mshindi kaa na udumu upande wa Mwenyezi Mungu ni mshindi kaa na udumu upande wa Mwenyezi Mungu. Daima Mwenyezi Mungu ni mshindi na ndiye humfanya anayemcha kuwa mshindi. Iwapo mambo yako hayaendi vizuri, labda mpangilio wa mambo yako wahitaji uchunguzi kila shida inalo suluhu yake.

Kutoka kwa maisha ya Yusufu twajifunza namna ya kumakinika katika utendaji wa mambo yetu, hata yakiwa magumu namna gani. Nasoma kutoka Mwanzo 41:25-45

Yusufu akamwambia Farao ndoto ya Farao ni moja tu. Mungu amemwonyesha Farao atakayofanya hivi karibu. Wale ng’ombe saba wema ni miaka saba. Ndoto ni moja. Na wale ng’ombe saba dhaifu wabaya waliopanda baada yao ni miaka saba nay ale masuke saba matupu yaliokaushwa na upepo wa mashariki yatakuwa miaka saba ya njaa. Ndivyo nilivyomwambia Farao ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayofanya hivi karibu.

Tazama miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya misri. Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake, na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya misri, na njaa itaiharibu nchi. Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye maana itakuwa nzito sana. Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili ni kwa sababu neon hilo Mungu amelithibitisha na Mungu atalitimiza upesi.

Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya misri. Farao na afanye hivi tena akaweke wasimamizi juu ya nchi na kutwaa sehemeu ya tano katika nchi ya misri, katika miaka hii saba ya kushiba. Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka ijayo saba ya njaa itakayo kuwa katika nchi ya misri nchi isiharibike kwa njaa. Neon hili likawa jema machoni pa watumwa wake wote. Farao atawaambia watumwa wake, tupate wapi mtu kama huyu mwenye roho ya Mungu ndani yake?

Farao akamwambia Yusufu kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote hapana mwenye akili na hekima kama wewe. Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu na kwa neon lako. Watu wangu watatawaliwa katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Farao akamwambia Yusufu tazama nimekuweka juu ya nchi yote ya misri. Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake akaitia mkononi mwa Yusufu akamvika mavazi ya kitani nzuri na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya misri. Farao akamwambia Yusufu mimi ni Farao na bila ya amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya misri. Farao akamwita Yusufu safenath panea, akamwoza asenathi binti Potifera kuhani wa Oni kuwa mkewe Yusufu akaenda huko katika nchi yote ya misri. Na huko katika nchi yote ya misri.

Maisha ya Yusufu yaonyesha wazi vile akili nzuri na njema hufanikishwa. Hebu na tupate ufafanuzi Zaidi. Baada ya Yusufu kupata habari zote kuhusu ndoto za Farao alimwambia Farao. Mst 28 “Mungu amemwonyesha Farao atakayofanya hivi karibu” Akamwambia miaka saba ya shibe itafuatwa na miaka saba ya njaa. Zaidi kwa vile ndoto zilikuwa mbili, na tafsiri ni moja, iliyonyesha ya kwamba ilibidi hali ile ichukuliwe kwa uzito, Zaidi maana ni mwenyezi Mungu alisema hayo. Akili nzuri ya Yusufu ilileta mafanikio kwa sababu, Mungu mwenye hekima yote alihuzinishwa. Heri kumhuzisha mungu katika hisia na fikra zetu n atutafanikiwa sisi binafsi na watu wetu n ahata nchi yetu, na katika shughuli zetu za kikanisa. Tujifunza kujiuliza swali hili. Je, mapenzi ya mungu ni yapi katika kila jambo, na mwenyezi mungu atatufanikisha, na tutakomaa katika akili zetu, na Zaidi tutawajibika na kupendeza katika jamii zetu. Neno lasema, mst 38 “Farao akawaambia watumwa wake, tupate wapi mtu kama huyu mwenye roho ya Mungu ndani yake?” Yusufu akapandishwa madaraka akawa mkuu wa nyumba ya Farao na katika utawala wan chi yote ya misri. Yusufu akazingatia yote ya kumcha mungu nayo mungu akamfanikisha. Heri wewe unayemhusisha mungu katika mipango yako, na kwa utukufu wake mwenyezi mungu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!