Tukeshe Katika Tumaini Letu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Tukeshe Katika Tumaini Letu
Loading
/
Mathayo 24:32-41

Habai. Ni wakati wa kujifunza neno la Mungu. Injili ya Mathayo 24:32-41. Tukeshe katika tumaini letu. Jina langu ni David Mungai. Baadhi ya watu wetu hujaribu sana kutuchangamshwa na ahadi za uongo. Ahadi tupu. Na huo huwa ndio mwisho wa matumaini yetu.

Bwana wetu Yesu Kristo, aliahidi na kutimiza. Pamoja na hayo Bwana wetu Yesu Kristo alisema mengi kuhusu tumaini letu a siku zijazo. Nasoma kutoka Injili ya Mathayo 24:32-41

Bwasi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likisha kuchipuka na kuchanua majani mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu. Nanyi kadhalika myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni. Amin nawaambia kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatakapotimia. Mbingu nan chi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna ajuaye hata malaika walio mbinguni, wala mwana ila baba peke yake. Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za nuhu ndivyo kutavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.

Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokutwa wakila na kunywa walioa na kuolewa hata siku ile alivyoingia Nuhu katika safina. Wakati ule watu wwili watakuwako kondeni, mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.

Katika fungu hili la neno la mungu twapata maneno ambayo kweli ni ya msaada kwetu kuangazia tumaini letu.
Maneno ndiyo haya

Uhakika

Siku na saa hazijulikani

Utengano

UHAKIKA: neno hili laamanisha kwamba tumaini letu katika Yesu Kristo ni kweli. Katika Mstari wa 33, tumesoma:
“Nanyi kadhalika myaonapo mambo hayo yote tambueni ya kuwa yu karibu milangoni.” Mambo hayo yametajwa kuanzia mstari wa 4-28. Kwa mfano, chikizo la uharibifu kwenye eneo la hekalu mjini yerusalemu. Hekalu liliharibiwa mnamo AD 70. Dhiki n ahata makristo wa uongo hayo ni dalili na ishara kwamba siku ya kiyama-kurudi kwake Yesu yakaribia na ni hakika kwamba tumaini letu, na kunyakuliwa la karibia. Na kwa sababu neno limesema kuwa hatujui siku wala saa, basi ni vyema tuwe tayari. Kama ilivyokuwa wakati wa nuhu, ndivyo itakavyokuwa na kuja kwake Yesu Kristo.

Wakati wa nuhu Maisha yalikuwa yaiendelea kawaida, na mvua ya gharika ikanyesha ikaungamza nchi kwa maji. Maisha yatakuwa yakiendelea kama kawaida na ghafla bin vuu parapanda ya kurudi kwake Yesu italia. Sauti ya malaika mkuu itasikika umeme na radi zitaonekana na mambo mengine kama hayo, na siku ya kiyama itafika. Usipomkubali Yesu Kristo kuwa mwokozi, sasa msikilizaji hautakuwa na nafasi wakati ule.

Pamoja na hayo, kweli kutakuwa na mambo ya kustaajabisha.

Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni, mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa mmoja aachwa. Kesheni basi, kwa maana hamjui ni siku ipi atakapokuja Bwana wetu

Dalili na ishara, twaziona basi hatuna budi kukesha.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!