Tujitayarishe Kwa Kurudi Kwake Yesu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Tujitayarishe Kwa Kurudi Kwake Yesu
Loading
/
Mathayo 24:42-51

Hujambo na karibu. Naitwa David Mungai na hiki ni kipindi cha matumaini. Leo twalitazama neno kutoka injili ya mathayo 24:41-51 ‘TUJITAYARISHE KWA KURUDI KWAKE YESU’.

Biblia yatufundisha tusifadhaikie kurudi kwake Yesu bali tusadiki hakika Yesu yuarudi tena. Nasoma kutoka Injili ya Mathayo 24:42-51

Kesheni basi kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamini neno hili; kama mwenye nyumba. Angaliijua ile zamu mwivi atakavyokuja angalikesha wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sabbau hiyo ninyi nani jiwekeni tayari kwa kuwa katika saa msiyodhani mwana wa Adamu yuaja.

Ni nami basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake awape watu chakula kwa wakati wake?

Heri mtumwa yule ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin nawaambieni atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake Bwana wangu anakawia, wajoli wake na kila na kunywa pamoja na walevi bwana wake mtumwa hiyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua. Atamkata vipande viwili. Na kumwekea fungu lake. Pamoja na wanafiki ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Kusema nasi kuhusu kurudi kwake mara ya pili Yesu alitoa mfano wa watumwa watatu

Mtumwa aliyekesha

Mtumwa mwenye hekima

Mtumwa muovu

Mtumwa aliyekesha ni mfano wetu wa kuwa tayari kwa sababu hatujui saa wala siku. Mungu kwa neema na huruma zake ameiweka siri ya kurudi kwake Bwana Yesu; tusije tukawa na uhakika, siku na saa ya kurudi kwake. Kama vile mwivi huja wakati asiyokuwa na kurudi kwa Yesu. Heri basi kwa yule anayekesha kiimani maana siku na saa, hakuna ajuaye.

Yesu akaendelea kusema mtumwa mwenye hekima aliyeweka mambo yote tayari maana wakati wo wote alimtaraji mwajiri bwana wake. Pamoja na hayo mtumwa mwema alikuwa mwaminifu kuyafanya mapenzi ya mwajiri wake, na kuyazingatia maagizo yake akiyatilia maanani aliyosema Mungu kwa mtumishi wake Musa.

Kitabu cha kutoka 3:11-12

Musa akamwambia mungu mimi ni nani hata niende kwa Farao nikawatoe wana wa Israeli watoke misri? Akasema bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika misri mtamwabudu mungu katika lima huu.
Maneno ndiyo hayo. “Bilas haka mimi nitakuwa pamoja nawe.”

Maneno hayo ni machache mno lakini yana maana au funzo la muhimu. Kwa kiebrania ni maneno manne tu na mungu alipoyasema maneno hayo Musa alikuwa katika shughuli zake za kila siku. Watu wengi wangedhani kwamba Musa alikuwa hekaluni mahali pa ibada. Hapana musa alikuwa katika shughuli zake za kawaida.

Na kwa huruma na neema yake mungu akamwambia. “Bilas haka mimi nitakuwa pamoja nawe.” Siyo lazima uwe kanisani ili mungu awe pamoja nawe. Kila wakati na po pote pale. Na ametuahidi kutujali po pote pale, hata atakaporudi na tutamwona na macho yetu. Kuna yule mtumishi mwovu ambaye hukaidi maagizo ya bwana wake na huendelea kutenda maovu, na mahali pa yule mtumwa ni pamoja na wanafiki na atupwa kweye kilio na kisaga meno.

Msikilizaji kesha na ujiweke tayari kwa kurudi kwake yesu, la sivyo utahesabiwa pamoja na wanafiki na hatimaye kutupwa kwenye kilio na kusaga meno. Mna tumaini la uzima wa milele kwa mumwamini yesu kristo. Bwana wtu Yesu Kristo yu arudi tena kutuchukua wote tunaomwamini.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!