Tabia Ya Mkristo

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Tabia Ya Mkristo
/
I Wakorintho 6:12-20

Hujambo na karbu. Tulichambue neno pamoja 1 Wakorintho 6:12-20

Jina langu ni David Mungai. Karibu, wombo kwanza halafu tuendelee.

WIMBO

Naam, karibu tena. Leo twalichambua kwa undani, makini, fungu la neno la Mungu kutoka 1 Wakorintho 6:12-20 ‘ tabia ya mkristo msikilizaji, bado twaishi katika ulimwengu wa dhambi, majaribu na masumbuko yatuzunguka. Twabanwa sana na tamaa za dunia, mwili na majaribu ya shetani. Hata hivyo, twahitaji kuishi juu ya hayo yote ndiposa Paulo, atuombea pamoja na wakristo wa Thessalonike 5:23
‘mungu wa Amani mwenyewe awatakase kabisa, nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu, mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo’

Sasa tunasoma, 1 Wakorintho 6:12-20

12 Vitu vyote ni halali kwangu lakini si vyote vifaavyo, vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu chochote

13 Vyakula ni kwa tumbo na tumbo ni kwa vyakula, lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye bwana ni kwa mwili

14 Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake

15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!

16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja?

17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye

18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake, ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.

19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe,

20 Maana minnunuliwa kwa thamani. Sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Ili tuweze kuwa na tabia njema kama wakristo, Paulo atukumbusha kweli tatu zinazohusu miili yetu. Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vifaavyo. Kwa mfano, ni halali kula nyama, kiasi, lakini usiwe mtumwa wa nyama.

Namjua daktarin mmoja Rafiki yangu, karibu afe kwa sababu ya kula nyama sana. Aipenda nyama, hii kwamba hakupendezwa na chakula kingine ila nyama. Siku moja kamwendea daktari mwenza, kupimwa, matokeo yakawa kwamba figo yake moja, karibu kufa. Akapewa dawa, na akaambiwa aache kuwa mtumwa wa nyama na kanywaji, ale mboga kwa muda bila nyama.

Baada wa miezi kadhaa, ya kula mboga, na kunywa maji, akapata nafuu. Una uhuru wa kulan a kunywa, lakini jiulize, Je, tabia hii yanifaidi nini? Je, yanifanya mtumwa, basi fanya kama ndugu yangu anayenifuata.

Josiah alikuwa mtumwa wa pombe, na katika kilabu moja, meza moja ilitengwa kwa ajili yake.

Tukaungama kitamilia kumwombea ndugu yangu kwa miaka mingi.

Siku moja ya siku kama kawaida alipitia pale kilabuni. Akaletewa chupa chake kama kawaida. Akazidharau akazisema ‘ Mr. Pombe, you have ruled over me ruthlessly and for many years, and from now on, I will never take you again’

Akasimama akaondoka hatimaye akamwamini Yesu Kristo, akaokolewa. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Ukweli wa pili, katika kanisa lile la korintho, baadhi ya washiriki walisema, kama vile chakula ni cha tumbo, ndivyo ilivyo na zinaa. Paulo basi aliwaonya na kuwaambia mwili si kwa zinaa bali ni kwa bwana naye bwana ni kwa mwili.

Na tumtukuze bwana kwa miili yetu. Neno lasema mst. 18
‘ikimbieni zinaa kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake, ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe’ ikimbie zinaa. Acha kucheza ramli na Maisha yako.
Ukweli wa tatu….mwili wako ni hekalu la roho mtakatifu aliye ndani yako, uliyepewa na mwenyezi Mungu.

Hekalu la Mungu,ni maskani yake Mungu, lilo kama lile hekalu lililokuwa korintho Aphrodite makao ya makahaba miili yetu ni makao mwa roho mtakatifu. Mwili wako si wa kila takataka ya ulimwengu bali ni makao ya roho mtakatifu huleta tunda, upendo, furaha, Amani, uvumilivu, utu wema, Fadhili, uaminifu, upole, kiasi, juu ya mambo kama haya hakuna sharia.

Na ukumbuke ya kuwa, bwana Yesu Kristo, ndiye aliyekukomboa. Je haujui ya kuwa mwili wako ni kiungo cha mwili, wa Kristo. Hivyo ndivyo ulivyo, na huo ndio ukweli wa mambo.