Sheria Ya Kuwajibika

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Sheria Ya Kuwajibika
/
I Wakorintho 4:1-5

Hujambo mpenzi msikilizaji. Natumai u buheri wa afya maana hiyo ndiyo furaha yetu. Jina langu ni David Mungai. Leo katika kipindi hiki cha MATUMAINI twalichambua fungu la neno kutoka 1 wakorintho 4:1-5.

Sheria ya kuwajibika ,wimbo halafu tuendelee.

Wimbo

Naam. Karibu tena. Tangu jadi siyo watu wengi hukubali kuwajibika au kukubali kwamba wamehusika, wengi hujiondoa.

Hawa alipotenda dhambi, alikataa kukubali, akamlaumu nyoka.

Haruni nduguye Musa, alipoongoza halaiki la watu kujitengenezea Mungu- sanamu; Musa aliposhuka kutoka Mlima Sinai, akamuuliza ndugu yake, Haruni, nini kilikuwa kikiendelea. Haruni alijibu akasema;
Kutoka 32:22 “Hasira ya Bwana wangu isiwake, wewe unawajua watu hawa ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya. “Haruni alijaribu kwepa na kulaumu watu wengine.

Mfalme Daudi alipolala na mke wa Uria, alijaribu kuepa Lakini wakati Nabii Nathani alikuja alimwambia mfalme Daudi maneno haya; 2 Samueli 12:7 “ Basi Nathani akamwambia Daudi, wewe ndiwe mtu huyo.”

Ni watu wachache sana hukubali wamekosea, bila kutoa au kujaribu kujitetea.

Ni kama vile unaweza kumkuta mtoto ala sukari mdomoni hata mikononi yaonekana wazi Lakini asisitiza kwamba hajaguza hiyo sukari. Twakataa kuwajibika na kulaumu watu wengine.

Tulitazame neno kutoka 1 wakorintho 4:1-5.

1 Mtu na atuhesabu hivi kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.

2 hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, Ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.

3 Lakini kwangu mimi si kitu kabisa nihukumiwe na nyinyi wala kwa hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hata nafsi yangu.

4 Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu Lakini sihesabihi haki kwa ajili hiyo, ila anihukumuye mimi ni Bwana.

5 Basi ninyi msihukumu Neno Kabla ya wakati wake hata ajapo Bwana ambaye atayamulikisha yaliyositirisha mashauri ya mioyo, ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.

Neno linasema ya kwamba sisi ni mawikili wa Bwana Yesu, na ni lazima tumtetee Yesu, na habari njema ya wokovu.

Lakini lazima, tuwajibike, tuwe makini kufanya na kusema yaliyo haki na kweli. Mstari wa 1-2 ‘ Mtu na atuhesabu hivi kuwa tu watumishi wa Kristo, na ma wakili wa siri za Mungu.

Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, Ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu, katika hali iwayo yote.
Akiwaandikia Waefeso, Paulo pia awaambia wakristo.

Waefeso 3:1-7

“kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenyu ninyi mataifa.

ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu,

kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache.

Kwa hayo myasomapo mtaweza kutambua ufahamu wangu, katika siri yake Kristo.

Siri Hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika roho.

ya kwamba mataifa ni warithi pamoja nasi katika urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake hiyo katika Kristo yesu kwa njia ya Injili.

7 Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji ya uweza wake na hata maneno ya mstari wa nane yaonyesha unyenyekevu wake Paulo. Katika huduma ya Mwenyezi Mungu.

Mtumishi na atumike kwa unyenyekevu, “mimi niliyemdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri mataifa utajiri wake Kristo Usiopimika.

Kwa unyenyekevu, Paulo aliwajibika mbele ya Bwana. Alimwakilisha Yesu, kama balozi wake hata kwa jela, kwa kuhubiri habari njema. Alijikabidhi mikononi mwake Mungu ahukumuye kwa haki, na kwa fadhili zake hakuna cha ziada, na kweli, Mungu ndiye aliye mkuu kulikowote.

Warumi 2:1-2;

“kwa hiyo, wewe mtu awaye yote ahukumuye, huna udhuru, kwa maana katika hayo umhukumuye mwingine wajihukumu mwenyeshe kuwa na hatia, kwa maana wewe uhukumuye unafanya yaleyale.

nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo.”

Na katika kitabu cha nabii Malaki 3:6 twasoma; “ kwa kuwa mimi, Bwana sina kegeugeu, ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo”

Mungu si kigeugeu, ni wa haki. Mungu ndiye atakayetoa hukumu ya kweli. Tuache kuhukumiana, hayo si yetu, maana hakuna atakayemkosoa Mungu. Kama mawakili wake Mungu, yetu kwa wakati huu ni kuwahubiria habari njema ya wokovu wa la si kuwahukumu.