Sahihisha Namna Unaishi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Sahihisha Namna Unaishi
Loading
/
I Wakorintho 15:29-34

Hujambo mpenzi msikilizaji. Natumai u buheri wa afya na karibu tujifunze Neno la Mungu pamoja. 1 Wakor. 15:29-34, “SAHIHISHA NAMNA UNAISHI”. Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu tena. Leo msikilizaji twalitazama fungu la Neno kutoka 1 Wakor. 15:29-34, “SAHIHISHA NAMNA UNAISHI”.

Ni muhimu kujua ya kwamba, neno lasema katika Warumi 14:12 “ Basi ni hivyo kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele yz Mungu.”

Na kunao wimbo, unaohimiza, ukweli huu na hata kumalizia na maneno;

“Siku hiyo itakuja
Kila mtu atauchukua, mzigo wake mwenyewee,
Na kila mtu atatoa, maneno yake mwenyewee,
Mbele za Mungu,
Siku hiyo inakuja.”

Nasoma fungu hili la Neno 1 Wakorintho 15:29-34

29 Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?

30 Na sisi kwa nini tumo hatarini kila saa?

31 Naam ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu, Bwana wetu ninakufa kila siku.

32 Ikiwa kwa jinsi ya kibinadamu nalipigana na hayawani wakati kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule na tunywe, maana kesho tutakufa.

33 Msidanganyike, mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

34 Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo, niwafedheheshe.

Katika maneno ya mstari wa 29-30. Paulo atufundisha ya kwamba; mtu asipoaamini ya kwamba, Kristo alikufa msalabani, akazikwa na siku ya tatu akafufuka, basi kubatizwa kwake hakuna maana.

Twajua hakika, kila mtu atakufa, lakini itakuaje baada ya kifo. Neno lasema katika Waeb. 9:27-28

27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu,

28 kadhalika Kristo naye akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.

Hebu tutazame maneno ya mstari wa 31

“Naam ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu, Bwana wetu ninakufa kila siku.”

Mara nyingi, Paulo alikuwa hatarini, kwa sababu ya kuhubiri Injili, na hii ndio sababu anatumia maneno “ ninakufa kila siku”. Paulo aliteswa sana, kwa sababu ya kuhubiri Injili ya Bwana, wetu Yesu Kristo.

Mateso tuyapata, tunapoihubiri Injili, lakini, tusihofu, maana mateso yetu, hayawezi kulinganishwa na utukufu tutakaopewa mbinguni.

Hata hivyo, mateso hayaleti faida, ye yote, tusipojitwalia, kwa Imani, kwamba mna ufufuo, baada ya kifo.

Na hilo ndilo tumaini. Basi na tushi kama watu walio na tumaini kla uzima wa milele mateso ni hapa hapa tu, kwa mkristo mbinguni ni uzima wa milele tukiwa pamoja na Bwana wetu Yesu Kristo.

Wakristo wa Korintho walikuwa na shida sana kuelewa na hayo, kama ilivyo na sisi.

Lakini ukweli ni kwamaba kama alivyokufa Yesu na kufufuka, ndivyo itakavyokuwa nasi pia. Kifo siyo mwisho wa anayemwamini Yesu, bali tuna ufufuo katika Kristo, na baada ya ufufuo, wetu na miili ya utkufu tutaishi na Yesu Kristo, milele na milele katika Ufalme wa Mungu Baba Yetu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!