Pokea Maradufu

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Pokea Maradufu
/
Mathayo 25:14-30

Hujambo! Naitwa David Mungai na ni furaha yangu kukuletea ‘matumaini.’ Tutalichambua neno pamoja. Injili ya Mathayo 25:14-30.

Wengi twashughulika kila siku tukitafuta Maisha mema. Maisha ya kukaa raha mstarehe na kusahau kunao Maisha ya siku zijazo n ahata Maisha ya milele na milele, kama yanavyoelezwa katika Injili ya Mathayo 25:14-30.

Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili na mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili na mmoja talanta moja kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake, akasafiri.

Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda akafanya biashara zao, akachuma faida talanta nyingine tano.

Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana yake. Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.

Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano akisema Bwana uliweka kwangu talanta tano, tazama talanta nyingine tano nilizopata faida. Bwana wake akamwambia vema mtumwa mwema na mwaminifu ulikuwa mwaminifu; kwa machache nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya Bwana wako.

Akaja na yule aliyepokea talanta mbili akasema Bwana uliweka kwangu talanta tano akaleta talanta nyingine tano akisema Bwana uliweka kwangu talanta tano tazama talanta nyingine tano nilizopata faida. Bwana wake akamwambia vema, mtumwa mwema na mwaminifu kwa machache nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya Bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta mbili akasema

Bwana uliweka kwangu talanta mbili tazama talanta nyingine mbili nilizopata faida. Bwana wake akamwambia vema, mtumwa mwema na mwaminifu ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema Bwana nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya, basi nikaogopa nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi wazama unayo iliyo yako. Bwana wake akajibu akamwambia wewe mtumwa mbaya na mlegevu ulijua ya kuwa navuna nisipopanda nakusanya nisipotawanya. Basi ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watu au riba nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

Basi mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa na kuongezewa tele, lakini asiye na kitu hata kile alicho nacho atanyanganywa. Na mtumwa yule asiyefaa mtupeni mbali katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Katika fungu hili la neno la mungu twaona ya kwamba mkubwa au boss wa watumwa wale aliwapa hela kulingana na uwezo wao wa kufanya kazi. Ni vyema na ni jambo la busara mtu kuujua uwezo na kipawa chako ili uweze kuongezea maarifa. Si vizuri kukwamia mahala pamoja. Ungezea maarifa. Watumwa wawili walipewa talanta. Wakwanza tano na wa pili mbili. Kwa bidi walifanya kazi. Wakaongezea maarifa katika ajira. Uendeleavyo kufanya hiyo kazi msikilizaji ndivyo utaendelea kupata maarifa na ujuzi wote wawili walifanya kazi kwa bidi wakaongezea mara mbili. Na bwana wao aliporudi aliwa[ongeza. Vema mtumwa mwema na mwaminifu..wakapongezwa maradufu na wakaupata wema kutoka kwa mwajiri wao. Uaminifu katika kazi yako ni muhimu sana. Usipokuwa mwangalifu katika ajira yako utamalizia vibaya kama yule mtumwa na boss alichofanya na talanta yake akasema

Nalitambua ya kuwa wewe ni mtu mgumu wavuna usipopanda wakusanya usipotawanya basi nikaogopa nikaenda nikaficha talanta yako katika ardhi, tazama unayo iliyo yako. Mwajiri alimkemea sana yule mtumwa, na kumwambia

Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; basi ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba. Nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. Basi mnyanganyeni talanta hiyo mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa na kuongezewa tele.

Acha uvivu, fanya kazi kwa badii na utaongezewa maradufu. Usipofanya kazi wakaa tu na ajira ipo, basi na kula usile. Fanya kazi kwa bidi utavuna unachopanda. Ujue talanta yako na uikuze. Hata wewe mtumishi wa Mungu, hubiri kwa bidi fundisha neno kwa bidi mshahara utapewa.