Paulo Awahimiza Wakorintho

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Paulo Awahimiza Wakorintho
Loading
/
II Wakorintho 6:11-18

Hujambo na karibu msikilizaji mpenzi. Natumai u buheri wa afya, na kwamba u tayari kujifunza Neno la Mungu pamoja nami. Leo twalitazama fungu hili la Neno kutoka 2 Wakor. 6:11-18. Paulo awahimiza Wakorintho. Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee

Naam. Karibu tena, tujifunze Neno pamoja.

Nasoma fungu hili: 2 Wakor 6:11-18

11 Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho, mioyo yetu imekunjuliwa.

12 Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu.

13 Basi, ili mlipe kadiri ile mliyopewa ( nasema nanyi kama na watoto), nanyi pia mkunjuliwe mioyo

14 Msifungwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawa sawa na kwa maana kuna urafiki gani kali ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja nay eye asiyeamini?

16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na Sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaaa ndani yao, na kati yao nitatembea, name nitakuwa Mungu wao, wao watakuwa watu wangu!

17 Kwa hiyo; Tokeni kati yyao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.

18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike. Asema Bwana mwenyeji.

Fungu hili la Neno la Mungu lina mafunzo mengi. Kwa mfano: Katika mstari wa 11, twaona ya kwamba, Paulo asema nao wazi, na Paulo na bundi lake, waliwaalika Wakorintho, na kuwapokea. Asema vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho mioyo yetu imekunjuliwa.

Na katika mstari was 14, twapata somo ambalo wengi wa Wakristo hawalipendi lakini ni muhimu.

“Msifungwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawa sawa na kwa maana kuna urafiki gani kali ya haki na uasi?”

Twauhusisha ukweli huu katika maisha ya ndoa, biashara, na uhusiano wetu na watu wengine.

Tujihadhari tusingizwe katika mambo yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.

Tukijihusisha na mabo yaliyo kinyume na Imani yetu, tutakuja juta baadaye.

Na hii ndiyo sababu, mstari wa 17 Paulo aendelea kufunza:

“…Tokeni kati yyao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike. Asema Bwana mwenyeji.”

Neno limesema tujihadhari tusitajwe tajwe pamoja na waharifu na wanaotajwa tajwa mtaani kwamba tabia zao zina kasoro. Na tusiyande ya ulimwengu kama linavyosema Neno katika 1 Yohana 2:15-17.

15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima havitokani na Baba bali vyatokana na dunia.

17 Na dunia inapita pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

Na zaidi, Neno lasema, tusiwe na ushirika na ndugu, walio na tabia ya kuishi katika dhambi: kama linavyosema katika 1 Wakorintho 5:11

“Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii, lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu”

Twaposoma kuonyesha mfano wa Kristo maishani mwetu kuachana kwa njia ya haki, kama tunavyowasoma Paulo na Barnabas walivyotengana kule Antonikia kwa sababu ya kijana Yohana aliyeitwa marko, baadaye waliurejesha uhusiano wao kama tunavyosoma katika kitabu cha Wakolosai 4:10

“Aristarko, aliyefungwa pamoja name, awasalimu na Marko mjomba wake Barnaba, mabaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni.”

Paulo aliyaandika maneno hayo kwa upendo. Hilo ni himizo la upendo.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!