Paulo Abadili Mpango Wa Safari Yake

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Paulo Abadili Mpango Wa Safari Yake
Loading
/
II Wakorintho 1:12-2:4

Hujambo na karibu, tujifunze Neno pamoja kutoka II Wakorintho 1:12-24. Paulo abadili mpango wa safari yake. Jina langu ni David Mungai. Karibu. Wimbo halafu tuendelee.

Naam na karibu tena tujifunze Neno pamoja II Wakorintho 1:12-24 “Paulo abadili mpango wa safari yake.” Kabla ya kusoma fungu hili la Neno, ni muhimu kujua ya kwamba, baada ya kuandika Waraka wa kwanza, Paulo alilitembelea kanisa la Korintho na akakuta ya kwamba kanisa lilikuwa limejichafua na mambo mengi mabaya. Na kwa sababu Wakorintho kuyatekeleza mashauri yake akaandika waraka mwingine kwa ukali na machungu mengi. Waraka huo, haukuwafikia washiriki wa kanisa; ukapotea, sura ya 10 mpaka 13 na ya 2 Wakorintho, ni sehemu ya waraka huo uliopotea ulikuwa waraka wa huzuni.
Huo ni utangulizi kwa kifupi sasa tuendelee, na somo letu la leo. Nasoma II Wakorintho 1:12-24

12 Kwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu si kwa hekima ya mwili bali kwa neema ya Mungu; tulienenda katika dunia na hasa kwenu ninyi.

13 Maana hatuwaandiki ninyi Neno, ila yale msomayo na kuyakiri, name nataraji ya kuwa mtayakiri hayo hata mwisho.

14 Vile vile kama mlivyokiri kwa sehemu ya kwamba sisi tu sababu ya kujisifu kwenu, kama ninyi mlivyo kwetu sisi, katika siku ile ya Bwana wetu Yesu.

15 Nami nikiwa na tumaini hilo halitaka kufika kwenu hapo kwanza ili mpate karama ya pili,

16 na kupita kwenu na kuendelea mpaka Makedonia kurudi kwenu na kusafirishwa nanyi kwenda Uyahudi.

17 Basi, nilipokusudia hayo, je! Nalitumia kigeugeu? Au hayo niyakusudiayo, nayakusudia kwa jinsi ya mwili kwamba iwwe hivi kwangu, kusema ndiyo, ndiyo na siyo siyo?

18 Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, Neno letu kwenu si ndiyo na siyo.

19 maana mwana wa Mungu Kristo Yesu aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa ndiyo na siyo bali katika yeye ni ndiyo.

20 Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo tena kwa hiyo katika yeye ni Amin. Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.

21 Basi yeye atufanyaye imara pamoja nanyi. Katika Kristo na kututia mafuta, ni Mungu.

22 naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa sabuni ya roho mioyoni mwetu.

23 Lakini mimi namwita Mungu awe shahidi juu ya roho yangu ya kwamba kwa kuwahurumia sijafika Korintho.

24 Si kwamba tunatawala imani yenu, bali tu wasaidizi wa furaha yenu, maana kwa imani yenu mnasimama.

Sura ya pili

1 Lakini nafsini mwangu nalikusudia hivi, nisije kwenu tena kwa huzuni.

2 Maana mimi nikiwatia huzuni, basi ni nani anifurahishaye mimi ila yeye ahuzunishaye name?

3 Nami naliwaandikia Neno lilo hilo, ili nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia nikiwatumaini ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia.

4 maaana katika dhiki nyingi na taabu ya moyo niliwaandikia na machozi mengi. Si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi.

Katika fungu hili la Neno la Mungu, Paulo alijitetea kwa nini alibadilisha safari yake kwenda Korintho.

Asije akawakasirisha Wakristo wa Korintho, Paulo atoa sababu ifuatavyo:

1 Paulo alitamani kutembelea Makedonia kwanza halafu aendelee na safari mpaka Korintho. Kama tunavyosoma katika I Wakorintho 16:5

I Wakorintho 16:5 Lakini nitakuja kwenu nikiisha kupita kati ya Makedonia, maana napita kati ya Makedonia.

Sababu ya pili, Paulo alibadilisha wa kusafiri kwenda Korintho kwanza asije akawatia Wakristo huzuni kwa sababu walikubalia dhambi itawale kanisa. Hali hiyo ingalimhuzunisha Paulo, na kanisa lote, maana

Paulo angewakemea vibaya. Paulo basi akachelewesha safari yake ili washiriki wa lile kanisa, wapate nafasi ya kuwarejesha walioangukia dhambini.

Somo kubwa kweli lazima tuwarejeshe walioangukia dhambini kwa upendo na hekima nyingi. Hatimaye Paulo alilitembelea kanisa la Korintho na kuwarejesha kwa upendo na kanisa likampa msaada wa kifedha apelekee kanisa la Yerusalemu. Twahitaji hekima katika kuwarejesha na ndugu waliwang’oa dhambini.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!