Ni Mungu Mmoja Tu Hutuhesabia Haki

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Ni Mungu Mmoja Tu Hutuhesabia Haki
/
Warumi 3:27-31

Hujambo na karibu. Ni Mungu mmoja tu anaye uweza wa kutuhesabia haki. Hiki ni kipindi cha matumaini. Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee

WIMBO

Naam na karibu tena. Twalichambua fungu la neno la Mungu kutoka wraka wa Paulo kwa Warumi 3:27-31 Dunia kote, wimbo ni dhambi na mambo yanayosababishwa na dhambi. Wanadamu tumeshindwa na ukweli ni kwamba , ni Mungu mmoja tu anayewezakutuhesabia haki. Twawezaje kuepuka mazao au matunda ya dhambi ? Sikiliza kwa makini linavyosema neno la Mungu.

Warumi 3:27-31

Basi, tunaweza kujivunia nini? Hakuna! Kwa nini? Je, kwa sababu ya kutimiza sheria? La! Bali kwa sababu tunaamini.

28 Maana Mungu humkubali mtu kuwa mwadilifu kwa imani, wala si kwa kutimiza matakwa ya sheria.

29 Au je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu, ama pia wa watu wa mataifa mengine? Naam, wa watu wa mataifa mengine pia.

30 Mungu ni mmoja, naye atawafanya Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.

31 Je, tunaitumia imani kuibatilisha sheria? Hata kidogo; bali tunaipa sheria thamani yake kamili.

Kutoka kwa sababu zilitowe na Paulo katika fungu hili la neno la Mungu twapata maelekezo kadhaa yanayomtukuza Mungu ambaye hutuhesabia haki.

 1. Hatupaswi kujisifu. Mstari wa 27.
  Basi, tunaweza kujivunia nini? Hakuna! Kwa nini? Je, kwa sababu ya kutimiza sheria? La!
  Bali kwa sababu tunaamini.
  Kujisifu ni adui, anakwamiza msururu wa neema ya Mungu na ambaye hutuhesabia haki kwa Imani , wala si kwa matendo uwekaji wa sharia na kadhalika. Kuburi na kujisifu hakitupeleki popote. Kuburi huja kabla ya kuanguka na Mungu humpinga aliye na kuburi.
 2. Watu wa mataifa, wamo kali ya wote wanaohesabiwa haki. Siyo lazima utahiriwe kimwili ili upate ondoleo la dhambi ni kwa kutubu kuungama dhambi sisi huhesabiwa haki. Mstari wa 30 Warumi 3:30
  Mungu ni mmoja, naye atawafanya Wayahudi kuwa waadilifu kwa imani yao, na watu wa mataifa mengine pia kwa imani yao.
  Kwa Imani katika Yesu Kristo sisi huhesabiwa haki. Ni kwa neema yake Mungu wala si kwa matendo. Matendo twayahitaji baada ya kumwamini Yesu Kristo moyoni- Matendo yahitajika ili kudhihirisha kuweka muhuri Imani yetu yaani tunayokiri kwa mdomo yetu, yaambatane na matendo yetu.
 3. Matakwa ya sharia yamekamilishwa katika Kristo. Msalabani Yesu alilia “Imekwisha” Akayakamilisha matakwa ya sharia kwa ajili na kwa niaba yetu. Kwa Imani katika Yesu, yote yametendeka na kukamilika. Maneno ya mst 31 ”Je, tunaitumia imani kuibatilisha sheria? Hata kidogo; bali tunaipa sheria thamani yake kamili.”
  Kwa kumuamin Yesu Kristo, yote ya wokovu wetu, yamedhibitishwa – yamewekwa
  muhuri kwamba yatosha.