Namna Ya Kukuzab Kanisa

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Namna Ya Kukuzab Kanisa
Loading
/
I Wakorintho 1:10-17

Natumai, u buhesi wa afya msikilizaji wangu po pote ulipo. Ni furaha yangu kukuletea kipindi hiki cha “Matumaini” leo twalichambua fungu la Neno la Mungu kutoka 1 Wakor. 1:10-17. “NAMNA YA KUKUZA KANISA”. Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

Wimbo

Naam- Karibu tena.

Katika Injili ya Mathayo 18: 19-20, tumeamriwa kueneza Injili na kuwafanya watu wanafunzi wa Yesu, na kuwabatiza. Katika 1 Wakor. 1:10-17, twaonyeshwa njia ya kuwakuza watu kiroho.
Ijapokuwa kunao watu, hasa katika nchi za magharibi. Wahimiza ya kwamba sisi twajenga falme duniani hii lakini Kristo ametuita sisi Wakristo tuujenga mwili wa Kristo. Kanisa kwa uenezaji wa Injili na kufundisha Neno la Mungu.

Nasoma fungu hili la Neno. 1 Wakor. 1:10-17

10 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana Ywesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri mija

11 Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe ya kwamba iko fitina kwenu.

12 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu kwenu husema, mimi niwa Paulo, na mimi ni wa Apolo, na mimi ni wa Kefa, na mimi ni wa Kristo.

13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

14 Namshukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo.

15 Mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu.

16 Tena naliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana, zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine.

17 Maana Kristo hakunituma ili nibatize bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika

Ili kanisa na Kristo, lipate kukua, Paulo ataoa mashauri kadhaa kwa Wakristo:

Lazima tutambue matendo na mambo yanayolikuza kanisa.

Lazima tujue na tukubali ya kwamba, tutafanya na kutenda yote kwa ajili ya mwokozi weyu Yesu Kristo.

Katika mambo yote tujue ya kwamba, Bwana wetu Yesu Kristo yu ndani na kati yetu. Na tukifanya hivyo, kwa utukufu wake Yesu, tujifunze kujiuliza, kimoyomoyo, kama Yesu Kristo anagalikuwa hapa, mwenyewe binafsi, Je, ningalisema, au Je ningalitenda haya? Je, ni maneno ya kujenga au ni ya kubomoa? Ni muhimu ni lazima tuukumbuke ukweli huu, kwamba, Yesu Kristo, ndiye Immanueli. Mungu pamoja nasi, na kama ni kukua kaika sherika zetu, twakua kwa jina na katika jina la Bwana wetu Yesu

Kristo, na si kwa utukufu wa Paulo au Apolo. Si kwa utukufu wetu binafsi, bali kwa utukufu wa Yesu Kristo, Bwana na mwokozi wetu.

Ukweli wa pili. Tuache kujiinua sisi wenyewe binafsi kama tunauyoma katika mstari wa 11-12.

“11 Kwa maana ndugu zangu nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.

12 Basi maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu husema mimi ni wa Paulo, na mimi ni wa Apolo, na mimi ni wa Kefa, na mimi ni wa Kristo.”

Tuache kujikweza wenyewe katika sharika zetu, tuweze kukua pamoja. Wimbo tumeuimba , tena sana. “ Ajikwezaye atashushwa, ajishushaje atakweza.”

Usiposikizana, na ndugu au dada, ni vyema kutafuta njia ya kuurejesha uhusiano na ushirika wenu katika Kristo. Kama ni lazima, ondoka, bila kupalilia masengenyo na fitina. Tukitofautiana kidogo, tusijenge milima ya fitina na masengenyo.

Jambo la tatu, tuache kuyachochea, na kuongezea chumvi yaliyo yetu binafsi. Mst 17 “ maana Kristo hakunituma ikli nibatize bali nihubiri Habari Njema wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo, usije ukabatilika. Yaani, yote aliyakamilisha Yesu msalabani, yasionekane kuwa si kitu. Hebu yafikirie yote yaliyompata Kristo bustanini mwa Gethsemane, kupelekea kwa wakuu wa dini na serikali; Kutemewa mate, kupigwa mijeledi, damu. Katililika alipochomwa ubavuni misumari miguuni itaji la miiba kichwani, uyabatilishe hayo yote kwa ajili ya sifa zako binafsi. Masha!

Daima twamhitaji Yesu, na ni muhimu tuwe wanyenyekevu kama Yohana Mbalizaji aliyesema:

“Yeye hana budi kuzidi bali mimi kupungua.” (Yohana 3:30)

Basi na tumpe Bwana Mungu azidi maishani mwetu, n ahata katika sherika zetu, tupate kukua pamoja.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!