Namna Ya Kujenga Kanisa

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Namna Ya Kujenga Kanisa
/
I Wakorintho 3:10-17

Natumai u buheri wa afya msikilizaji wangu. Leo twalichamua neno kutoka 1 WAKORINTHO 3:10-17, ‘Namna ya kujenga kanisa’

Jina langu ni David Mungai, wimbo halafu tuendelee

WIMBO

Naam, karibu tena. Twalichambua fungu la neno kutoka 1 WAKORINTHO 3:10-17

Siku hizi karibu madhehebu yetu yote, huweka mkakati wa sera za kuanzisha na kujenga makanisa sehemu mbalimbali. Ni jambo nzuri lakini kunayo mambo kadha wa kadha tunapaswa kukumbuka,

Mjengo hutegemea msingi, msingi wa kanisa ni Yesu Kristo.

Uzuri na umaridadi wa jingo hutegemea mbao au mawe unayoyatumia.

Mjengo wa kanisa la kiroho la wakristo wote, uwepo wa roho mtakatifu ni lazima.
Hebu tusome,

10 ‘kwa kadiri ya neema ya Mungu, niliyopewa mimi, kama mkuu wa wajenzi wenye hekima, naliuweka msingi na mtu mwingine anajenga juu yake, lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake

11 maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani Yesu Kristo

12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri

13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto wenyewe utaijaribu kazi ya mtu, ni ya namna gani

14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa atapata thawabu

15 Kazi ya mtu ikiteketea atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa, lakini ni kama kwa moto

16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo, kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu ambalo ninyi…

Fungu hili laangazia kiti cha Kristo(Bema) atakapotuzawadi sote, wakristo kulingana na kazi zetu. Kazi na matendo yanayoangaziwa si ya wokovu bali ni ya baada ya kuokolewa kwa mtu kama inavyoelezwa Zaidi katika 2 wakr 5:10, Ni wakristo pekee wanaotajwa hapa.

Kiti hiki cha hukumu ya Kristo hutajwa kwa jina linguine (bema)tutatunukiwa

Taji ya haki kwa wote wanaopenda kufunuliwa kwake Yesu 2 tim 4:8

Taji kwa wale wanawavuta wengi kwa Kristo 1 wathess 2:19

Taji ya uzima alivyowaahidia wote wampendao Yesu yakobo 1:12

Taji ya waumini wanaoteswa, taji ya uzima ufunuo 2:10

Taji ya utukufu kwa wachungaji wa kanisa 1 petero 5:4

Matendo na kazi na huduma zetu zitapitishwa kama kwa moto, za dhahabu na mawe, zitajimudu lakini za miti na nyasi zitaungua na itakuwa hasara, kama tunavyosoma maneno ya mstari wa 15
1 wakorintho 3:15

Kazi ya mtu ikiteketea atapata hasara, lakini yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama moto

Jambo linguine, na ni ukweli muhimu sana ni kwamba , kanisa la Mungu linaloundwa na kila anayemwamini Yesu Kristo kwa hiyo twapaswa kujua kanisa ni maskani mwake Roho Mtakatifu

1 wakr 6:19

‘au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yenu mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe’

Nikiwa mkristo, lazima kwa unyenyekevu nimtambue Yesu Kristo aliye msingi wa Imani yangu. Lazima nijitoe kwake aniunde kiroho nikue, katika hali ya kuhudumu, nikule chakula kigumu cha neno, ili kanisa lake Mungu likue na kusimama imara