Namna Usawa Maishani

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Namna Usawa Maishani
Loading
/
Mathayo 23:23-28

Habari na hujambo msikilizaji. Karibu tujifunze neno la mungu katika kipindi hiki cha matumaini. Leo twalitazama neno kutoka Injili ya mathayo 23:23-28. Jina langu ni David Mungai.

Katika fungu hili la neno la mungu, twaona ya kwamba namna usawa wa Maisha. Kuishi Maisha ya usawa ni vigumu maana katika hali nyingi hayutoshani. Na katika Injili ya Mathayo 23:23-28 Yesu aeleza hivi:

Ole wenu waandishi na mafarisyao wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira lakini mmeacha mambo makuu ya sharia, yaani adili na rehema na Imani, hayo imewapasa kuyasanya wala yale mengine msiyaache!viongozi vipofu wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano na ndani yake vimejaa unyanganyi na kutokuwa na kiasi. Ewe farisayo kipofu safisha kwanza ndani ya kikombe ili nje yako nayo ipate kuwa safi.

Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri bali ndani yamejaa mifupa ya wafu na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki bali ndani mmejaa unafiki na maasi. Mambo yasiyo ya kawaida tunayofanya ni matunda au mazao ya Maisha yetu yasiyo ya kawaida. Mafarisayo na waandishi walijua ya kwamba torati na sharia zilitoa masharti kwamba watoe sehemu ya kumi ya kila kitu lakini walitoa nusu nusu wakijifanya hawakumbuki. Mambo muhimu wakayayeyusha na kuwa kama ya kawaida. Maisha yakawa ya kuyumba yumba, kwa hatari kuu. Si mbele na si nyuma. Si moto si baridi. Hekaheka tu sisizoweza kueleweka.

Ndipo wakapewa mfano wa kikombe waliosha kikombe juu na ndani ni chafu. Hivyo ndivyo hali ya dini isiyo na Kristo ni kuishi tu bila hata utaratibu.

Ndipo Yesu akawaambia Heri kusafisha ndani kwanza na kufuatanisha na usafi wa nje; yaani usafi wa kusamehewa dhambi kwa kutubu kuungama na kughairi mioyo na Maisha yetu kuwa na uhusiano mwema na mungu, na kwa fadhili na neema yake hutusamehe dhambi zetu, nayo matendo ya Maisha hutia muhuri kwamba twaufurahia wokovu wetu, kwa sabbau kwa Imani tu warithi wa uzima wa milele katika Yesu Kristo. Yesu Kristo amekuwa Mwokozi na Mkombozi wetu. Amekuwa Immanueli Mungu pamoja nami/nasi. Hata siku ya kiyama.

Imekuwa na hata wakati tumesongwa na kubanwa sana na mambo na changamoto maishani, Bwana wetu Yesu Kristo bado ndiye mchugaji mwema anayetufunza hata tunapoishiwa na nguvu n ahata uwezo maishani.

Mimi ni mshahidi wa hayo. Kwamba mimi kama kondoo wake Yesu hunichunga. Siku moja nilikuwa naishiwa kweli sikuwa n apes ahata ya kutoka afisini kwenda nikaomba kimoyoyo. Mungu wangu kweli wajua sitaki na naona vibaya kuuliza mtu anipe msaada. Nakuomba unipe pesa za kutoa katika duka la mpesa lililo karibu sana na afisi yako. Ilikuwa Jumamosi tarehe 17 Dec, baada ya maombi mimi nikaendelea kuandika ujumbe wa kipindi cha matumaini-muda si muda simu ikalia unknown number simu ya pili ikalia nikaona ujumbe umepokea

Ksh……kutoka kwa Fulani nchini uingereza. Mungu ana uweza wa kutoa amri kwa ajili yako na lazima kuisalimu amri Heri anayeosha Maisha yake kutoka na ndani na hali ya kiroho hujitokezea na kuonekana katika Maisha ya nje kwa maneno na vitendo. Tusiwe wanafiki kama mafarisayo waandishi na masadukayo, walioosha Maisha nje na ndani ni chafu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!