Namna Mungu Ataifunga Historia – Part 2

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Namna Mungu Ataifunga Historia - Part 2
Loading
/
Danieli 9:20-27

Hujambo. Leo twalichambua neno la Mungu kutoka DANIELI 9:20-27

Jina langu ni David Mungai, karibu wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam, karibu tena tujifunze pamoja Neno la Mungu kutoka kwa chou cha nabii Danieli 9:20-27

20 basi hapo nilipokuwa nikisema na kuomba na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za Bwana Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu

21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuimba, mtu yule Gabrieli niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.

22 akaniagiza, akaongea nami akasema, Ee Danieli nimetokea sasa,ili nikupe akili upate ufahamu.

23 mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari, maana wewe unapendwa sana, basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya

24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na (to make an end of sin) kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu

25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuijenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu, kutakuwa na majuma saba, na katika majuma sitini, na mawili utajengwa tena pamoja, na njia kuu zake na handaki (wall), naam katika nyakati za taabu.

26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakataliwa mbali, naye atakuwa hana kitu na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika na hata mwisho ule vita vitakuwapo, ukiwa umekwisha kukusudiwa

27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja, na kwa nusu ya juma hiyo, ataikomesha sadaka na dhabihu, na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu na huyo hata ukome, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwaga juu yake mwenye kuharibu

Katika aya ya 27 twapata habari za dhiki kuu. Ni dhiki kuu maana itakuwa na mahangaiko mengi pale mwanzoni wa dhiki, ya juma moja au miaka saba, mpinga Kristo atawashawishi waisraeli wawe na pango wa Amani naye, eti awasaidie kuleta Amani. Baada ya miaka mitatu u nusu, yule mpinga Kristo, atayavunja yale makubaliano maana atamani kuabudiwa kama Mungu. Waisraeli watakataa na wengi watauawa. Funzo hili pia latajwa katika injili ya Mathayo 24:15 na 2 Thessalonika 2:4

Nasoma Mathayo 24:15 ‘na hapo mtakapoliana chukizo la uharibifu lile lililonenwa na nabii Danieli limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu)

Neno hili chukizo latoa maana ya yule mtu wa dhambi, Mpinga Kristo ambaye atakiuka maagaano yake na waisraeli, baada ya miaka 3 ½ ya dhiki na kuwataka waisraeli na dunia yote imwabudu, kama Mungu.

Watakaokataa Mpinga Kristo atawauwa kwa sababu ya Imani yao.

Mtume Paulo, atia muhuri fundisho hili alipowaandikia waumini wa kanisa la Thessalonike 2 Wath 2:4

Yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa, hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu’

Na mauaji hayo yatafika kilele chake, kwa kurudi tena kwake Yesu mara ya pili, kwa kishindo kama mfalme wa wafalme wote duniani, kuwapinga Mpinga Kristo na watu wake. Muuaji ya wapiga vita kutoka nchi mbali mbali watauwawa, na Kristo atakuwa mshindi na kutawala kwa miaka elfu, na kuendelea milele, pamoja na Mungu mbinguni.

Lakini lijue mwisho wetu waweza kuja mapema kuliko vile tulivyodhania.

Suleimani atushauri hivi, Mhubiri 12:13-14

13 Hii ndiyo jumla ya maneno, yote yamekwisha sikiwa, mche Mungu, nawe uzishike amri zake maana kwa jumla ndiyo impasavyo mtu’

14 Kwa maana Mungu ataleta hukumu kila kazi pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya’

Mwamini Yesu, upate wokovu maana chochote chaweza kutokea.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!