Mwendo Katika Upya Wa Uzima

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mwendo Katika Upya Wa Uzima
Loading
/
Warumi 6:1-7

Hujambo na karibu. Leo katika matumaini twalichambua fungu la neno la mungu, Warumi 6:1-7 mwenendo katika upya wa uzima. Jina langu ni david mungai, wimbo lafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena

Siku moja mama mungai alikwenda shambani akamkuta mtoto wa swara amelala fofofo. Akamshika akamleta nymbani akampa maziwa ya ng’ombe kila siku. Mtoto wa swara akawa likini hakuruhusiwa kutoka nje. Aliwekwa ndani ya chumba chake kila wakati. Anatembea anarudi anatembea ana rudi anafika mwisho wa chumba chake anarudi. Aendi popote

Maisha yetu hayapaswi kuwa vile. Mwendo wetu katika Maisha yetu mapya katika kristo yanapaswa kuwa na maendeleo kiroho. Maelekezo tumepewa katika waraka wa Paulo kwa warumi 6:1-7 nasoma

1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?

2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?

3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?

4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;

6 mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;

7 kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.

Kutoka kwa fungu hili, Paulo atuhimiza

  1. Hata tupo katika hali na wakati wa neema ya mungu na husamehewa dhambi tunapotubu basi
    twahimizwa tusiendelee kutenda dhambi. Hapo awali katika sura ya tano aya ya ishirini twapata
    maneno haya
    Laikini sharia iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana na dhambi ilipozidi neema ilikuwa nyingi Zaidi

Na hapa katika sura hhii ya sita mstari wa kwanza twasoma

1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?

Hatupaswi kusamehewa dhambi na kuenenda katika dambi tena

Himizo la pili katika aya ya tau ubatizo humaanisha kwamba tumeunganishwa na kristo katika kifo chake. Ni pale msalabani tuliondolewa dhambi na tunapoenda katika dhambi na kumsuluisha yes umara tena na tena na tamhuzunisha roho wa mungu aliyendani yetu. Miili yetu yapsawa kuwa hekalu lake roho mtakatifu na tunapoendelea na dhambi roho mtakatifu haha uhuru tena kufanya kazi na tunda la roho maishani mwetu halipo

Himizo la tatu; twahimizwa kuenenda katka kristo na mwishoni tutafufuliwa pamoja naye katika ubatizo, twafa na kufufuliwa pamoja na kristo maana utu wa kale ulisulibiwa pamoja na kristo msatari wa sita,

6 mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;

7 kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.

Soma na ulikariri neno lake mwenyezi mugu Biblia. Litafakari jitwalie ahadi upatacho nenoni mwake mungu maana tukisimama katika ahadi zake mungu tutakuwa washindi maishani.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!