Mungu Hutibu Dhambi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu Hutibu Dhambi
Loading
/
Warumi 5:12-21

Hujambo na karibu. Leo katika matumaini twalichambua fungu la neno la mungu kutoka Warumi 5:12-21 mungu ndiye hutibu dhambi. Jina lanf]gu ni David Mungai wimbo alafu uendelee

Wimbo

Naam karibu tena katika kipindi cha matumaini

Kunayo magonjwa na maradhi ambayo madaktari hawajapta tiba kuna maradhi mengine dawa ni tele na hupatikana lakini kuna magonjwa ambayo madaktari hawana tiba. Ugonjwa wa dhambi hauna tiba kutoka kwa madaktari. Ni mung utu aliye na tiba ya dhambi. Nasoma kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 5:12-21

12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;

13 maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria;

14 walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.

15 Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.

16 Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki.

17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.

18 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.

19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.

20 Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;

21 ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.

Ili tuweze kuelewa na tiba ya dhambi lazima tuelewe na kweli kadhaa zinazohusu dhambi

Dhambi lilkuwa na mwanzo. Kwa mmoja dhambi iliingia ulimwenguni. Adamu na hawa walinaswa na mtego wa shetani pale bustani ya edeni na sote tu wenye dhambi maana tu uzao wa adamu na mshahara wa dhambi ni mauti na huo ndio ukweli wa mambo.

Pamoja na hayo ni vyema tujue ya kwamba kama vile dhambi iliingia kwa mtu mmoja kuhesabiwa kulikuja kwa mmoja na ndiye yesu kristo aliposulubiwa pale msalabani hivyo ndivyo tumesoma katika mstari wa 15 na 16 kipawa cha haki kitatawala kwa yeyote anayemwamini yesu kristo mungu hawezi kumhesabu mtu haki asipomwamini. Yesu kristo moyoni. Zaidi sana tuujue ukweli wa neema yake mungu. Kwa kifupi, kwa neema yake yesu na kumwamini mungu hutufanya watoto wake na warithi wa ahadi zake mungu, uzima wa milele na kungojea tena kwa hamu kurudi kwake yes umara ya pili.

Kwa vitendo vyetu hatuwezi kushuhudia wokovu kwa sababu ya neema yake mungu twapata wokovu bila malipo na matendo kwa Imani pekee twapata wokovu. Hatuwezi kujivunia vitendo vyetu havina uweza wa kutupatia wokovu. Vitend hufwatana na kitabu cha yakobo, huwa dhihirisho thibitishi la wokovu wetu, kwamba mtu akimwamini yesu amebadilishwa kuwa mtu mwema na hubadilishwa na mwenyezi mungu kuwa vyema kuliko hapo mbeleni

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!