Mungu Ataikamilisha Historia Ya Binadamu – Part 1

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Mungu Ataikamilisha Historia Ya Binadamu - Part 1
Loading
/
Danieli 9:20-27

Natumai u buheri wa afya msikilisaji na Karibu tujifunze Neno pamoja. Jina langu ni David Mungai, na leo twalitazama Neno kutoka Danieli 9:20-27, namna Mungu ataikamilisha sahihi historia ya binadamu. Karibu wimbo halafu tuendelee na Neno.

Wimbo

Naam, Karibu tena tujifunze neno pamoja Danieli 9:20-27- namna Mungu ataikamilisha historia yetu- yaani Historia yetu sisi wanadamu.

Katika maneno ya mstari wa 24, twapata unabii, uliotabiriwa waisraeli na Danieli, unabii wa majuma sabini, ambayo yakijumlishwa huwa miaka 490. Unabii uliyopo hapa wahusu taifa la Israeli tangu wakati wa ujenzi wa ukuta wa Yerusalemu, na unabii huu waendelea mpaka kurudi kwake Yesu Kristo mara ya Pili baada ya ule wakati wa dhiki kuu.

Kila juma katika unabii huu- kila juma ni wakati wa miaka saba kwa hiyo majuma saba ni miaka 490. Katika unabii huu, na kulingana na maneno ya mstari wa 24, twapata mambo sita; nasoma sikiza vizuri, “Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako na juu ya mji wako takatifu. Ili (1) kukomesha makosa. (2) Kuishiliza dhambi, (3) Kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu (4) Kuleta haki ya milele (5) Kutia muhuri maono na unabii (6) Kumtia mafuta aliye mtakatifu.
Mambo hayo sita hayatakamilishwa mpaka ifike, kikomoni.

Kwa kifupi- miaka 483, imeisha. Ilianza na kujengwa kwa ukuta wakati wa Nehemiah na kuishia na kusulubiwa na kufufuka kwake Yesu.

Kati ya juma la 69 na 70 mna pengo la juma moja na pengo hilo ni wakati wa neema- wakati wa kumwamini yesu Kristo. Juma la saba litaanza baada ya kunyakuliwa kwa wanaomwamini Yesu Kristo kuwa mwokozi wao.

Juma hili la mwisho litakuwa na wakati wa kuteswa kwa waisraeli, na mwisho dhiki kuu.

Halafu Yesu atarudi awapiganie waisraeli na kupata ushindi dhidi ya majeshi makali kutoka kaskazini, kusini, mashariki.

Kwa sasa tuna uhakika juma la 70 bado na bado ni wakati wa kulihuri Neno la Mungu na mlango wa kuingia zizini la kondoo wa Mungu ni wazi.

Siku yaja ambayo nafasi haitakuwa. Ndiyo sababu ya maneno ya Mstari 27 yasema…

“Naye atafanya agano thibiti na watu wengi kwa muda wa juma ( miaka saba) na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka ya dhahabu, na mahali pale litasimama chukizo la uharibifu na hivyo, hata ukomo na ghadhabu iliyokusudiwa imemwaga juu yake mwenye kuharibu”

Juma hili la sabini litakuwa na mambo mengi sana, kama yanavyoelezwa katika Injili ya matayo, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake alipokuwa mlimani wa Oliveti.

Pia Paulo, alilitaja wazo au funzo hili katika wathesalonike 2:1-12 na ufunuo sura ya 6-19. Mengi maovu yatatendeka kwenye miaka saba ya dhiki.

Na kama nilivyotangulia kusema- Juma hili la sabini litafikia mwisho kwa kurudi kwake Kristo mara ya pili kwa kishindo, kupiga, vita na kupata ushindi na kuanzisha ufalme wake wa miaka elfu kumbuka ya kwamba, ikawa ilivyosema neno, tutatawala pamoja naye Bwana wetu Yesu Kristo.

2 Timotheo: 11-13 “Ni Neno la kuaminiwa kwa maana, kama tukifa pamoja naye Kristo, tutaishi pamoja naye pia… Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye…kama tukimkana Yeye, Yeye naye atatukana sisi…Kama sisi hatuamini, Yeye hudumu wa kuaminiwa kwa maana hawezi kujikana mwenyewe”

Na huu siyo mwisho wa mambo. Paulo anamhimiza na kumshauri Timotheo.

Mstari wa 14. 2 Timotheo 2:14

Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu,

Nasi twakukumbusha hayo msikilizaji, hayo ya unabii, upate nguvu na ujasiri katika safari hii ya kwenda Mbinguni na unabii wa Danieli wahimiza na kuhakikisha ukweli huu. Na Hivyo Mungu ataikamilisha Historia ya Dunia Je u tayari

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!