Meza Ya Bwana 2

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Meza Ya Bwana 2
/
I Wakorintho 11:17-34

Natumai u buheri wa afya msikilizaji wangu mpenzi, na ni furaha yetu kukuletea kipindi hiki cha matumaini. Leo twalichambua fungu la Neno la Mungu kutoka 1 Wakorintho 11:17-34 “MEZA YA BWANA”

Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo, halafu tuendelee.

Naam tuendelee kulichambua Neno. 1 Wakorintho 11: 17-34. Namna ya kujiandaa kushiriki “Meza ya Bwana”. Madhehebu tofauti ya Kikristo hushiriki katika “Meza ya Bwana”; siku tofauti kila juma, zingine kuandaa Meza ya Bwana, mara kadha kila mwezi. La muhimu ni kujua na kukumbuka ya kwamba katika “meza ya Bwana,” sisi huadhimisha kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo. Bwana wetu Yesu Kristo yu hai.

Nasoma fungu hili la Neno 1 Wakorintho 11:17-34

17 Lakini katika kuagiza haya, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara.

18 Kwa maana kwanza mkutanapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu, nami nusu nasadiki.

19 Kwa maana, lazima kuwapo na uzushi kwenu, ili waliokubaliwa wawe Dhahiri kwenu.

20 Basi mkutanipo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana;

21 Kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa.

22 Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.

23 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,

24 naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huyu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.

26 Maana kila mwalapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

27 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana, isivyostahili atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.

28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.

29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutopambanua ule mwili.

30 Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadhaa wa kadha wamelala.

31 Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa.

32 Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia.

33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanipo mpate kula mngojeaneni,

34 mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake, msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliyosalia nijapo nitayatengeneza.

Kutoka fungu hili la Neno la Mungu twapata mashauri kadhaa ya msaada katika kushiriki katika meza ya Bwana.

Katika mstari wa 20, twapata maneno haya: “Basi mkutanipo yaani mabo ya kuangalia kwa makini katika kushiriki Meza ya Bwana.”

Zamani zile, Wakristo washirikiana katika karamu za upendo, waliposhirikiana kuchanga pesa kwa wale hawajiwezi kimaisha.

Pia walitumia wakati ule kuwasiliana; kupata habari za makanisa mengine ya eneo lao. Pia walikumbuka wajane na mayatima.

Baadhi yao walikuwa matajiri, na walikataa kuwashirikisha wengine chakula chao, kwa hiyo kwa haraka walikula chakula chao kabla kuwahi kwa wengine. Basi Paulo akawashauri kwa maneno ya mstari wa 22.

“Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.”

Wakati wa kumkumbuka Yesu Kristo na kifo chake msalabani, si wakati wa kuonyesha, utajiri na ukuu wetu binafsi.

Jambo la pili. Tunapoumega mkate, humkumbuka Yesu, na vile aliteseka msalabani na kulimwaga damu yake kwa kuoshwa kwa dhambi zetu na hiyo damu. Twapaswa kufanya hayo, kwa heshima na unyenyekevu, na sifa nyingi kwa kusamehewa dhambi zetu. Sisi ni wanadamu, na hiyo damu hutuosha kabisa.

Mstari wa 28 na 31 yatauonya.

“Lakini mtu ajihoji mwenyewe na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. (31) Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa.”

Pamoja na hayo tuule mwili wa Kristo kwa adabu njema, na kwa heshima.

Natufanye hivyo, mpaka kurudi kwake Yesu Kristo. Tumsifu na kumshukuru kwa upendo wake, kajitoa kufa wa msabalani.