Matumaini Ya Leo

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Matumaini Ya Leo
Loading
/
II Wakorintho 2:5-17

Hujambo na Karibu. Leo twalichambua fungu la Neno la Mungu kutoka 2 Wakorintho 2:5-17. Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo, halafu tuendelee

Naam wimbo wa kuburudisha kweli. Leo kama nilivyotangulia kusema. somo letu lapatikana katika 2 Wakorintho 2:5-17. Tutaligawa fungu hili katika sehemu mbili,

Mstari 5-11- Fungu lafundisha namna ilivyo muhimu kumsamehe mwenye dhambi.

Mstari 12-17, Namna tunavyoweza kupata ushindi katika Kristo.

Tuanze na fungu la kwanza Mstari wa 5-11- ni muhimu kumsamehe mwenye dhambi. Nasoma;

5 Lakini iwapo mtu amemhuzunisha, nakunihuzunisha mimi tu, bali kwa sehemu (nisije nikalemea mno), amewahuzunisha ninyi nyote.

6 yamtosha mtu wa namna hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi.

7 hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi.

8 kwa hiyo nawasihi kumdhibitishia upendo wenu

9 maana naliandika, kwa sababu hii pia ili nipate bayana kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote.

10 Lakini kama mkisamehe mtu neno lolote, nami nimemsamehe, kwa maana mimi nami ikiwa nimemsamehe mtu neno lolote nimemsamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo.

11 Shetani asije akapata kutushinda kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.

Ni muhimu kumsamehe ndugu au dada katika Kristo tusimupe shetani nafasi ya kutuhangaisha.

Sehemu ya pili; Mstari 12-17. Namna tunavyoweza kupata ushindi. Nasoma; 2 Wakorintho 2:12-17;

12 basi nilipofika Troa, kwa ajili ya Kristo, nikafunguliwa mlango katika Bwana,

13 Sikuona raha nafsini mwangu kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali naliagana nao, nikaondoka kwanda Makedonia.

14 ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu yakumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu

15 kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea.

16 katika hao, wa pili harufu ya mauti iletayo mauti, katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo

17 Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu, bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu twanena katika Kristo.

Paulo, alikuwa hana pumziko la moyoni, kwa sababu Tito alikosa kumfikia apate kujua hali ya wakristo katika kanisa la Wakorintho.

Licha ya huduma nzuri Troa ambapo watu walimwamini yesu – Paulo alikuwa na huzuni maana hakujua hali ya ndugu Tito, na kanisa la korintho. Paulo aliwajali na kuwafikiri watu wengine, katika zizi la Kristo.

Kama Paulo, naomba tuwajali ndugu na dada katika shirika zetu.

Na katika mstari wa 14, twapata maneno haya.

“ila Mungu ashukuriwe, anayetushungiliza,Daima katika Kristo na kuidhihirisha harufu yakumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.

Katika fungu hili, twamwona Mungu na Ushindi wake, na astahili sifa zetu.

Naye Bwana wetu Yesu Kristo, ndiye Jemedari mkuu maana ndiye ndiye aliyemtwaa Paulo na kumfanya mtumwa wake, na kwa furaha, Mungu amtumikisha Paulo kama inavyoonekana katika waraka huu wote.

Na kwa sababu ya ushindi huo, harufu tamu duniani na Mbinguni kwa wale wanaookoka kwa kumwamini Yesu Kristo.

Ni harafu ya dhabahu zinazompendeza Mungu, kwake Mungu dhabihu za mwili yetu na hata harufu cha kifo chake Msalabani.

Na harufu ya ufufuo wa Yesu Kristo na zaidi harufu ya ufufuo wetu katika Kristo Yesu, na kuingia katika ufalme wa Mungu milele na milele, licha ya shida na taabu tunapokuwa duniani hii.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!