Matokeo Ya Wivu – Part 1

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Matokeo Ya Wivu – Part 1
/
Mwanzo 37:12-28

Hujambo mpendwa msikilizaji, na karibu tujifunze neno la mungu katika kipindi hiki cha matumaini. Leo twalichambua neno kutoka kitabu cha mwanzo 37:12-28. Jina langu ni David Mungai. Na kichwa cha mafunzo yetu ni; matokeo ya wivu. Nasoma kutoka Mwanzo 37:12-28

“Reubeni akawaambia, msimwage damu, mtupeni katika birika hii iliyopo nyikani wala msimguse. Ili apate kumwokoa katika mikoni yao, akamrudishe kwa baba yake. Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa. Wakamtwaa, wakamtupa katika birika, na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji. Nao wakakaa kitako kula chakula. Wakainua macho yao wakaona msafara wa waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane wakisafiri kuvichukua mpaka misri. Yuda akawaambia ndugu zake na kuificha damu yake? Haya na tumuuze kwa hawa waishameli wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu. Ndugu zake wakakubali. Wakapita wafanya biashara wamidiani basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika wakamwuza Yusufu kwa frdha ishirini na wakachukua Yusufu mpaka Misri.”

Ndugu zake Yusufu walikuwa machungani. Yusufu alikuwa nyumbani na babake alikuwa mpendwa wa babake. Babake alikuwa amemshonea kanzu maridadi, na ilionekana akiwa mbaali. Kwa siku nyingi babake hakujua habari za wanawe machungani. Akamtuma Yusufu akawajulie hali ndugu zake waliokuwa machungani. Alikosa njia kidogo lakini akaelekezwa walimokuwa ndugu zake. Alipokuwa mbali, ndugu zake wakamwona anatembea pole pole, tayari amevalia kanzu yake maridadi wakamwonea wivu, na mara moja wakapendekeza kumtenda Yusufu maovu. Mmoja wa ndugu zake alipendekeza wamuue, wamtupe ndani ya shimo halafu wamchinje mnyama watumbukize nguo yake kwa damu halafu wamwambie baba yao kwamba Yusufu kauawa na mnyama. Ni wivu unaopofusha macho ya dhamiri wivi kama ule hupovusha n ahata maono. Hujui unaenda mbele au nyumba lakini hawakuacha kutafuta njia na mbinu za kumuangamiza Yusufu.

Wakasema, tusiue, lakini tumweke ndani ya shimo, na tumwache pale afe. Hawakuona kama ni hatia kufanya hivyo. Reubeni mwana wa kwanza aliwambia, “ tusimwage damu” reuben alikuwa mwana wa kwanza wa mke wa yakobo wa kwanza. Naye Yusufu alikuwa wa kwanza wa mke wa pili- kwa jina Raheli. Labda Reubeni alifikiria labda angerudishwa mbaraka wa kwanza, lakini mambo hayakuwa hivyo. Kwa hiyo, akapendekeza wasimuue yusufu bali wamtupe shimoni akiwa shimoni atajiua kwa mateso ndani ya shimo. Wivu huua watu na wenye kutenda hayo matendo maovu. Tumeyasoma magazetini waume wamewaua wake zao kwa sabbau ya wivu, waajiri na walioajiriwa hali ni iyo iyo.

Wivi husababisha mabaya maishani mwetu. Mithali 6:34 “maana wivu ni ghadhabu ya mtu. Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisazi.” Wivu ni mbaya. Pendekezo la tatu: tumuuze Wakakubaliana kwamba wamuuze Yusufu. Yuda ndiye aliyependekeza hivyo, na akasema maneno ya busara. Heri tungekuwa na wachache waaminifu katika nchi, wangesema kama Yuda mst 27 “haya na tumwuze kwa hawa waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali”

Kama tungalikuwa na wachache wanaozingatia maneno ya Yuda maafa yangepungua, na hatimaye yaishe. Mikono yetu isiwadhuru wengine maana ni ndugu zetu; waishameli ni wa aina nyingi tuwaachie kutekeleza hayo, lakini tusihesabiwe pamoja na wale wanaomwaga damu za ndugu zao, kabila zote za nchi hii sisi ni ndugu, basin a tuishi kw aundungu na ujirani mwema, maana hayo ndiyo mapenzi ya mungu. Walimuuza ndugu yao kama mtumwa na ndiye aliyewaokoa na njaa baadaye.

Wivu ni kosa na dhambi na ni heri kujiepusha nao, na tujikabidhi kwake mungu maana ndiye hujishughulisha saana na mambo yetu. “ Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu. Msaada utakaonekan atele wakati wa mateso. Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, mungu wa yakobo n ngome yetu. Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, mungu wa yakobo ni ngombe yangu. Kwa sharti na ni muhimu kumkabidhi mungu fadhaa zetu zote kwa sababu tayari anajishughulisha sana nazo.