Matendo mema huelekeza wapi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Matendo mema huelekeza wapi
Loading
/
Mwanzo 5:21-24

Hujambo na karibu. Leo twalipata neno letu kutoka Mwanzo 5:21-24. Je, matendo mema hutuelekeza wapi? Jina langu ni David Mungai. hakuna mtu duniani asiyejua mema na maovu. Kila nchi duniani ina sharia zake, kwa wananchi wote. Hata watu wasio na ustaarabu wanao sharia zao za kuwaongoza kama jamii. Familia n ahata dini mbalimbali zina sharia zao. Tumeumbwa kwa njia ya kipekee inayotuelekeza katika tabia ya kuishi vyema. Na hata hutuonyesha namna ya kutenda mema. Na hatuwezi kutenda mema tusipokuwa na uhusiano mwema mmoja na mwingine. Katika majadiliano yetu tutaona vile tunaweza kuwa na uhusiano mwema na Mungu. Na hilo ndilo swali twapaswa kujibu? Maisha mema hutuelekeza wapi? Hebu tumchunguze Henoko, labda twaweza kupata jibu. Nasoma kutoka Mwanzo 5:21-25

“Henoko akaishi miaka sitini na mitano akamzaa methuselah. Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa methuselah miaka mia tatu, akazaa wana waume na wa kike. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu naye akatoweka maana Mungu alimtwaa”


Henoko ni mfano mzuri wa kuiga maana alikuwa mtu kama sisi maana alimpendeza Mungu maishani mwake. Watu wengi na dini mbalimbali hupendekeza maisha ya kujinyima waweza kuwa na ushirika wa karibu na Mungu lakini Henoko alikuwa kama sisi watu wa kawaida, lakini Neno la Mungu lasema. “Henoko akaenda pamoja na Mungu”

Henoko alikuwa mtu wa kawaida. Alikuwa na mke na akaishi katika jamii na akaenda na Mungu. Watu wengi huwaogofya vijana kwamba maisha ndoa ni magumu. Sikatai lakini ukiishi na kuenenda na Mungu, itakuwa tofauti kinachosababisha changamoto ni kukataa kuwa changamoto ni kukataa kuwa changamoto ni kukataa kuwa wanyenyekevu kila mmoja ataka mambo yake yafuatwe. Barabarani waendeshaji wa magari wasipopeana nafasi husababisha msongamano wa magari. Vivyo hivyo tusipomruhusu Roho wa Mungu kufanya kazi maishani mwetu tutaleta kazi maishani mwetu tutaleta msongamano maishani mwetu. Tamaa zetu na za dunia zitakuwa zikishindana mioyoni mwetu na husababisha msongamani nayo Amani ya moyoni haupo. Henoko alienenda na Mungu kwa sababu alikuwa na ushirika mwema tena wa karibu na Mungu.

Pia twaona ya kwamba Henoko alikuwa wa jamii ya Nuhu. Nuhu alihubiri injili ya haki kwa miaka mia moja na ishirini. Hali kadhalika Henoko alijitoa kwake Mungu kwa unyenyekevu, ndiposa Mungu akamkweza kwa njia zake na kwa wakati wake. Henoko alienda na Mungu kwa miaka mia tatu, baada ya kumzaa methuselah. Kushirikiana na Mungu kila siku humfanya mtu kutunukiwa na Mwenyezi Mungu. Na hata akachukuliwa mbinguni bila kufa. Wengi walikufa lakini Henoko alichukuliwa mbinguni akiwa hai. Tukiishi maisha ya haki tutazawadiwa na kukaribibishwa mbinguni maskani yake Mwenyezi Mungu.

Mungu awatafuta watu wa kuenenda nao. Sio lazima uwe spesheli bali uwe mnyenyekevu. Je, wewe u mmoja wao. Jihadhari sana na wandani wako.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!