Matarajio Yetu Mambo Yakiharibika

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Matarajio Yetu Mambo Yakiharibika
/
Mathayo 24:29-31

Hujambo msikilizaji. Leo katika matumaini twalichambua neno kutoka Injili ya Mathayo 24:29-31 mambo yakiharibika tifanyaje? Jina langu ni David Mungai.

Biblia yatufunza na kutufahamisha habari za Mwokozi aliyeimwaga damu yake kwa kifo cha msalaba ili tupate ondoleo la dhambi. Kufufuka kwake pia, ni muhimu. Ndiyo sababu sisi husherehekea pasaka. Ingawa alijitoa akauchukia mwili wa kibinadamu Yesu Kristo hakutenda dhambi baada y kufufuliwa kutoka kw wafu alipaa mbinguni na sasa ameketi mkoni na sasa ameketi mkononi mwa mungu wa kuume akituombea. Na katika fungu hili la neno la mungu injili ya Mathayo 24:29-31 twapata habari na mafundisho ya kurudi kwake disho ya kurudi kwake esu mara ya pili. Injili ya Mathayo 24:29-31

Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni na nguvu za mbinguni zitatikisika. Ndipo itakapoonekana ishara yake mwana wa Adamu mbinguni, ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakaoomboleza, nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti ya parapanda nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.

Swali Je, Yesu Kristo atarudi kwa nguvu? Ndiyo atarudi kwa nguvu maana kutakuwepo mambo matatu yatayohusu na nguvu kuambatana kurudi kwake.

Mabadiliko mbinguni. Tumesoma Yesu akisema, “Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga wake na nyota zitaanguka mbinguni na nguvu za mbinguni zitatikisika.” Kuna mara nyingine jua lilitiwa giza siku ile Bwana wetu Yesu Kristo alisulibiwa msalabani. Jua lilitiwa giza kuanzia saa sita mchana mpaka saa tisa. Mwezi hautatoa mwanga kwa sabbau mwezi hupewa mwanga na jua. Nyota zote zitaanguka kutoka mbinguni lakini Yesu alisema.“ lakini mara baada ya dhiki kutakuwa mabadiliko makuu mbinguni. Nguvu za mbinguni zitalikisika kweli, Yesu Kristo atarudi kwa nguvu.

Ishara. Yesu akasema. “ndipo itakapoonekana ishara yake mwana wa adamu mbinguni ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza na wao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

Bwana wetu, Yesu Kristo kama alivyopaa kurudi mbinguni akionekana katika wingu ndivyo atakavyo rudi duniani juu ya mawingu nasoma kutoka matendo ya mitume 1:9-11.

Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama akainunuliwa wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe. Wakasema enyi watu wa galilaya mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni. Atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Mambo ni wazi. Namna alivyopaa mbinguni ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo atarudi. Wateule. Katika mstari wa 31 twasoma. Nye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.

Malaika ni watumishi wake Yesu Kristo watatumwa ulimwenguni wote kuwakusanya wote wanaomwamini Yesu. Parapanda itapigwa nao malaika watatumwa, kuwakusanya wateule wa Bwana Yesu Kristo. Yesu kristo atatoa amri, na malaika zake watafanya hiyo kazi. Wanaomwamini Yesu wote watakusanywa pamoja na kurudi kwake Yesu kutajawa na nguvu na utukufu.

Hayo matatu yatakuwa wazi katika kurudi kwake Yesu. Kama alivyosema yesu kristo, itakuwa hivyo kwa sabbay yesu kristo ni mungu. Basi tuwe tayari kwa kumwamini na kumpokea mioyoni mwetu.