Maswali Maalum

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Maswali Maalum
Loading
/
Mathayo 22:41-46

Hujambo. Hiki ni kipindi cha matumaini na katika kipindi hiki, sisi hujifunza neno la mungu. Leo twajifunza kutoka Injili ya Mathayo 22:41-46. Hapa twapata maswali maalum kweli. Jina langu ni David Mungai. Kunao maswali ambayo kweli huwezi kupata majibu haraka tena kw aupesi, maana mambo hubadilika na wakati , lakini maswali ya kiroho hupata jibu kwa ukweli usiobadilika. Katika Injili ya mathayo 22:41-46 Yesu aliuliza maswali ya muhimu sana, na tutayatafakari katika kipindi hiki. Nasoma kutoka Injili ya Mathayo 22:41-46

Na mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza akisema, mwaonaje katika habari za Kristo? Ni mwana wa nani? Wakamwambia, ni wa Daudi. Akawauliza imekuaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana akisema, Bwana alimwambia Bwana wangu, uketi mkono wangu wa kiume hata niwawekapo adui zako kuwa chini ya miguu yako? Basi Daudi akimwita Bwana amekuwaje ni mwanawe? Wala hakuweza mtu kumjibu neno, wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena” Maswali makali tena maalum. Kwa mfano Kristo ni mwana wa nani? Jina Kristo kw akigiriki ni Christos na maana kwa kiebrania ni masihi kwa hiyo swali lilikuwa Kristo ni mwana na nani? Na Mesiya ni mwana wa nani? Msikilizaji Maisha yetu ya sasa, nay a milele yategemea namna tunajibu swali hili. Kristo ni mwana wa nani?

Jibu la swali hili ni la muhimu kabisa, na kweli walitoa jibu sahihi. Walisema “Ni mwana wa Daudi”. Naye Yesu akawauliza imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana? Ni muhimu kwa sababu jibu la swali hili huleta maana ya Maisha ya milele na milele. Swali ni hili. Kwa nini Daudi alimwita Yesu Bwana? Katika Roho Daudi aliandika. Zaburi ya 110 “Neno la Bwana kwa Bwana wangu uketi mkono wangu wa kiume; hata ni wafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako”

Neno BWANA ukiona limeandikwa kwa herufu kubwa humaanisha YEHOVA mkombozi wa Israeli aketiye mkononi wa mungu wa kuume-mesiya amewekwa mahali pa mamlaka pamoja na mungu Baba. Pia tumesoma maneno haya “hata niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako” hayo ni ya wakati ujao.

Yamaanisha ya kwamba wakati wa ufalme wake Yesu wa miaka 1000, watu wa mungu watajitoa kumfuata Yesu Kristo. Naye Kristo atatuongoza kwa Amani adilifu. Amani iliyokomaa. Hii ndiyo sababu Daudi akamwita Mesiya, BWANA miaka karne kumi kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo. Na hii ndiyo sababu hata Daudi alimwita BWANA hata kabla ya kuzaliwa kwake. Yesu ni Bwana na pia ni mwana wa mungu. Hiyo ni siri kuu na ni kweli. Alijitolea kuuvaa mwili wa kibinadamu ili hatimaye aangikwe na mwili wake pale msalabani kwa ajili ya dhambi zetu fidia ya dhambi akalipa ili tukimwamini tuwe huru na tabia za dhambi tamaa za dunia na za kimwili. Mungu aliupanga mpangilio wa wokovu wako tangu jadi. Ni kutubu dhambi kuungama na kumwamini Yesu na kughairi mwenendo na wokovu upate. Ni nani huyu Yesu Kristo, ni Mwokozi na Bwana wa kila amwaminiye na anaemwamini anao uzima wa milele. Yesu akiwa Mungu, alijitoa kwa ajili yetu. Yu heri anayemwamini Yesu Kristo akawa mkombozi na mwokozi.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!