Makusudi Ya Mungu Kwetu

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Makusudi Ya Mungu Kwetu
/
Warumi 8:28-30

Hujambo na karibu

Makusudi ya mungu kwetu ni yapi? Neno la mungu latoa jibu. Usibadilishe mtambo tegea hapo upate jibu jina langu ni David mungai, kipindi ni matumaini wimbo alafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena. Ni yapi makusudi ya mungu kwetu? Waanzilishi wote wa mambo wao uwa na makusudi akilini mwao. Mtu hawezi akiwa na akili timamu hawezi kuanza safari asipojua anasafiri kwenda wapi

Twajua mungu ndiye mwanzilishi wa uu,baji wa vitu vyote na aliumba vyote na aliumba vyote akiwa na makusudi yake. Mungu alituumba akiwa na makusudi flani na maalum kwetu na apenda kutekeleza makusudi hayo kwetu bila shaka. Sasa nasoma fungu la neno, Warumi 8:28-30

28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.

Mungu anayo makusudi matatu kwetu

Kusudi la kwanza mungu ataka tujue maneno ya mstari wa 28

28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Atamani tuwe watu waliojua neno na ujuzi wa neno hutuongoza katika hamu na hekima mungu ataka tujue kwamba katika mabo yote mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendaye yaan wale walioitwa kwa kusudi lake

Ni kusudi lake mwenyezi mungu tujue na kusadiki kuwa wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafanishwe na mfano wa mwana wake ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi

Heri mkristo ajuaye kwamba tangu jadi mungu alikujua na kwa jina ni mapenzi yake ujue na uishi ukijua hivyo kwamba muumba wako alikujua tangu asili alikuumba kwa njia ya kuogofya na njia ya kutisha na akakuuba upya katika kristo akakufanya kiumbe kipya akakufanya hekalu la roho mtakatifu maskani mwake mungu mweza yote kusudi umwakilishe hapa duniani kwa ushuhuda wa maneno yako na matendo yako mungu amekuita kwa kusudi lake sikiliza tena maneno ya mstari wa 30

30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.

Kwa wakorintho Paulo aliwaambia kwamba mungu atutukuza kwa utukufu milele na milele na milele tutaishi katika utukufu wake mungu na milele alipo bwana wetu yesu kristo. Swali ni hili tutajitwalia ukweli huu hamna gani

Makusudi yake mungu kwetu tutajitwalia kwa kujitoa kwake yesu na kumpokea moyoni maana yesu ndiye njia ya pekee ya kuingia mbinguni makao ya mungu

Kwa Imani mpokee yesu kristo moyoni na utakuwa mmoja wa wale wanaoyajua makusudi yake mungu