Kwanini Torati

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Kwanini Torati
Loading
/
Wagalatia 3:19-25

Hujambo msikilizaji karibu tulichambue neno waraka wa Paulo kwa wagalatia 3:19-25, kwanini torati? Jina langu ni david mungai wimbo halafu tuendelee

Karibu tena tujifunze neno katika mafunzo ya neno la mugnu twajua na kufahamu ya kwamba mungu ni mungu wa torati na ana utaratibu kwa mfano jua huchomoza kati siku na usiku kwa wakati wake zote mbili hazijitokezi kwa wakati mmoja kweli mungu ana torati na sharia zake na utaratibu.

Jadwali na orodha hazina kasoro kwanini mungu akatoa torati kwa mkono wa musa? Mtume Paulo aliyefahamu neno bado auliza swali hilo katika waraka wapaulo kwa wagalatia 3:19-25

19 Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe.

20 Basi aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja.

21 Basi je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria.

22 Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.

23 Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.

24 Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.

25 Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi.

Kwanini torati? Majibu anayo yatoa Paulo katika fungu hili la neno yatusaidiakujua mungu ndiye aliyetoa torati katika agano la kale katika biblia ya kiebrania mungu alitumia maneno 95 kueleza dhambi ni nini na katika agano jipya mungu ametumia maneno 28 kueleza dhambi ni nini torati basi imemweka kiwango flani ili tujue mema na mabaya torati huonyesha kiwango cha utakatifu wake mungu ambacho hakuna mtu anao uwezo wa kuweka na mtu akiweka toratisote ukavunja moja umevunja zote na hukumu ni hii

Mshahara wa mauti ni dhambi na mauti lakini karama ya mungu ni uzima wa milele katika kristo yesu

Pamoja na hayo torati ni mwalimu na njia ya kutufikisha kwake yesu kristo sote tumefikisha kwake yesu kristo. Sote tumeivunja sharia na torati lakini ni mmoja tu aliyeiweka sharia hii na kikamilifu na si mwingine kwa hiyo tunapomwam9ni yesu kristo kwa Imani hukamilisha matakwa yote ya sharia na kuhesabiwa haki Mbele zake mungu na kukombolewa kutoka kwa nuvu za ndhambi Bwana wetu na asifiwe milele a milel kwa iimani katika kristo yesu tumehesabiwa haki

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!