Kusudi La Sheria

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Kusudi La Sheria
/
Warumi 7:7-14

Hujambo msikilizaji naitwa david mungai na ni furaha yangu kukuletea kipindi cha matumaini. Leo twalichamua neno la mungu kutoka warumi 7:7-14 kusudi la sheria. Furahia wimbo huu alafu tuendelee.

Wimbo

Naam karibu tena. Leo tunapolichambua neno la mungu bibila, twapata mawazo yake mungu maana kama nabii isaya amesema, Kamba vile mbingu ipo mbali na dunia ndivyo na akili zetu hutofautiana na za mungu.

Lakini tunaposoma neno la mungu na kujitwalia ahadi zake mungu basi twapata kujua mawazo na makusudi yake. Lakini kwanini mungu kampa musa torati? Twapata jibu kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 7:7-14

7 Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.

8 Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.

9 Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa.

10 Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti.

11 Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, na kwa hiyo ikaniua.

12 Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.

13 Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.

14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.

Kusudi la kwanza la sheria ni kwamba sheria hufafanua dhambi. Sheria hutuonyesha lililo bayan a makossa. Twajua kuua ni makossa na ni dhambi. Maana sheria imesema usiuesheria ni mwalimu, hufafanua dhambi tupate kujua

Sheria huvumbua dhambi, kwa kuisha mioyoni mwetu tamaa ya kutenda dhambi. Dhambi inapovumbuliwa basi mioyo na akili hutamani na kuvutiwa kutenda. Paulo afafanua ukweli huu hivi

9 Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa.

10 Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti.

Sheria hutoa mwelekeo wa dhambi. Sheria ni takatifu lakini pia yaonyesha ukiweka yote na kukosa katika moja umevunja yote. Ndio maana Paulo ashangaa na kusema;

13 Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.

14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.

Kwa hiyo lazima tuelewe ya kwamba mungu aliitoa sheria ili sheria ituelekeze katika kuwa na uhusiano mwema na mungu, lakini sisi kwa uweza na nguvu za kimwili hatuna uwezo. Mungu hakuchoka nasi bali alimtoa nyesu kristo ili kwa kifo chake cha msalaba ya kamilisha yote ya sheria ili tukimpokea yesu kristo mioyoni mwetu kwa kutubu, kuungama na kumkiri tupate ondoleo la hukumu ya sheria.