Kufahamu Yasiyojulikana

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Kufahamu Yasiyojulikana
/
I Wakorintho 2:11-16

Hujambo na karibu, tujifunze Neno pamoja, 1 Wakor. 2:11-16 “KUFAHAMU YASIYOJULIKANA.” Jina langu ni David Mungai. Karibu wimbo, halafu tuendelee.

WIMBO

Naam. Karibu tena. Kufahamu yasiyojulikana. Akili zetu ni kama bahari ambayo huwezi kufikia au kufahamu kina kilia chake.

Wengi wamejaribu kuelewa akili za binadamu lakini bado waendelea na uchunguzi. Lakini twawezaje kujua yasiyojulikana? Nasoma kutoka 1 Wakor. 2:11-16:

11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila roho wa Mungu.

12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia bali roho atokaye kwa Mungu, maksudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

13 Nayo twanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya Rohoni

14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu, maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni

15 lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu

16 maana, Ni nani aliyefahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia.

Hapa msikilizaji, twapata ushauri wa Paulo kwa kanisa la Korintho. Paulo alijua, Wakristro wa Korintho walikuwa wanajaribu kuyaelewa ya kiroho kwa fikira zao za kimwili. Ni shida, Roho mtakatifu asipotafsiri na kutusaidia kuelewa kama tunavyoona katika maneno ya mst.13.

Ni jambo ngumu kutafsiri mambo na mafundisho ya kiroho kwa fikira za binadamu. Nekodemo hangeweza kuelewa, maana ya kuzaliwa mara ya pili. Ilikuwa ni lazima apate waidizi kutoka kwa Roho Mtakatifu. Na wahubiri wa Neno sharti tuelewe na hayo, tusishangae nasipoelewa. Ni kumwachia Roho wa Mungu afanye kazi yake, kama vikle maneno ya mstari wa 13 yanafundisha.

Yanayofundishwa na Roho na kuyafasiri mambo ya rohoni, kwa maneno ya rohoni. Kutafsiri ya roho, kwa ajili ya akili za kiroho.

Kwa hiyo, ukitumia akili za kibinadamu huwezi kuelewa wala kufahamu.

Ukweli huu ilikuwa ndani ya Paulo sana, maana na hata alipowaandikia Wakristo wa kanisa la Rumi aliwaambia hivi katika warumi 8:9

“Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili, bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote, asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.”

Na katika waraka huu wa 1 Wakor. 2:15 twapata fungu la maneno haya:

“Lakini mtu wa rohoni, maana yake ni kwamba, Mkristo anayeamirika; aliye jasiri, anayeongozwa na kufundishwa na Roho wa Mungu; hufurahia yote yaliyo mtukuza Mungu.”

Anaweza kuyaelewa, akiongozwa na Roho, anayeongozwa na akili, na hisia za kibinadamu, hawezi kuyaelewa kweli au maagizo ya Neno la Mungu.

Mkristo, anayeongozwa na Roho wa Mungu, hulitazama Neno, akitaka kujua ukweli wa mambo.

Kwa mfano, kwa nini Mkristo, anayeongozwa na Roho wa Mungu hapaswi kushiriki katika mambo ya uchawi. Kwa sababu Neno lasema: (Wagalalia 5: 19-21)

19 Basi matendo ya mwili ni Dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi.

21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufaklme wa Mungu.

Mkristo aliyeongozwa na Roho wa Mungu ni rafiki wa Neno la mungu. Maana Neno humpa mkristo, mwelekezo.

Eneza Injili ndiyo, fundisha Neno, ndiyo, lakini mwachie Roho wa Mungu, azae matunda maishani mwa mwenzako/ wenzako.

Pia mwachie Roho wa Mungu akuongoze akitumia Neno la Mungu unapolisoma. Kazi ya Roho wa mungu ni kweli, kamilifu na haki.

Watu watakucheka, lakini si kupenda kwao, ni kwa sababu hawaelewi ya kiroho.

Nakuombea, uijue mipaka ya kiroho na kimwili.

Uelewe, akili za kimwili haziwezi kuelewa ya kiroho.

Nakushauri kumhusisha Kristo akilini mwako, kwa na katika maisha yako. Yafikiri sana hayo niyasemayo na Mungu atakupa akili katika mabo yake.