Kilio Usiku Wa Manane

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Kilio Usiku Wa Manane
Loading
/
Mathayo 25:1-13

Hujambo na karibu. Leo katika matumaini twayachambua maneno yanayopatikana kutoka Injili ya Mathayo 25:1-13 ‘ KILIO CHA USIKU WA MANANE’. Jina langu ni David Mungai.

Kwa kunao mambo katika Maisha na kwa kweli hatujui mwisho wa hayo mambo. Tungependa sana kuyajua ya kesho. Lakini huo uwezo hatuna na kwa sababu hatujui ya kesho ni vyema kuwa tayari cho chote chaweza kutokea. Katika Injili ya mathayo 25:1-13 twasoma ya arusi

Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi waliotwaa taa zao wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu na watano wenye hasara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao wasitwae na mafuta pamoja nao, bali wale wenye busara walitwa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane pakawa na kelele, haya bwana arusi tokeni twende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote wakazitendegeza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara. Tupeni mafuta yenu kidogo. Maana taa zetu zinazimika.

Lakini wale wenye busara wakawajibu wakisema, sivyo hayatatutosha sisi na ninyi afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao mkajinunulie. Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naya arusini, mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine wakasema Bwana Bwana utufungulie. Akajibu aksema, amin nawaambia, siwajui ninyi. Basi kesheni kwa sababu hamwijui siku wala saa.

Harusi inayotajwa hapa yafunza kwamba wanawali wote kumi walikwenda kuwalaki Bwana na Bi Arusi. Na wote kumi walibeba zao. Bwana asema kwamba watano wao walikuwa wenye busara na watano walikuwa wapumbavu, kwa sababu walikosa kuweka mafuta ya kutosha katika taa zao, na kwa sababu arusi ilikawishwa basi mafuta yao yakaisha.

Wanawali wenye busara walijaza taa zao mafuta. Walikuwa tayari kabisa, wote walikwenda kumlaki Bwana Arusi.

Bwana arusi alipokawia kufika wanawali wote wakachoka wakalala. Wakasinzia wakalala usingizi. Ingawa wenye busara walibeba mafuta kiasi wote walikwenda kumlaki Bwana arusi. Bwana arusi alikawia sana. Na wote walisinzia na wakalala. Heri tujifunza na kuwa tayari kwa Imani hata aje Bwana arusi-Yesu Kristo.

Pia, lazima tukumbuke wanawali wale wapumbavu walichelewa kabisa wakafungiwa nje. Walibisha na kuitana. “Bwana Bwana utufungulie akajibu akasema Amin nawaambia siwajui ninyi.” Walichelewa kwa sababu walikwenda kununua mafuta hali wamechelewa wangenunua mafuta mapema. Yatupasa kufanya mambo kwa wakati unaofaa, la sivyo tutaishi kuchelewa. Fanya mambo wakati unaofaa la sivyo tutaishi kuchelewa. Fanya mambo wakati unaifaa usije ukakosa kufanikiwa. Fungu hili la neno la mungu lamalizia kwa maneno haya “Basi kesheni kwa sababu hamwijui siku wala saa.”

Wanawali wote walitamani kumwona na kumlaki Bwana Arusi. Ingekuwa heri kama wote wangeingia katika harusi, lakini wale wapumbavu waliachwa nje. Kilio kwamba kilisikka usiku wa manane wakati ambao hawakutarajia.

Nakusihi msikilizaji uwe tayari nyakati zote maana hatujui siku wala saa ya kurudi kwake Yesu Kristo. Twajitayarisha kwa kumpokea Bwana wetu Yesu Kristo, kwa Imani mioyoni mwetu. Na Zaidi tudumu katika hiyo Imani.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!