Kanuni Za Utoaji

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Kanuni Za Utoaji
/
II Wakorintho 8:16-9:5

Natumai u buheri wa afya msikilizaji mpenzi. Karibu tujifunze neno la Mungu pamoja. Leo twalichambua neno la Mungu kutoka 2 Wakorintho 8:16-9:5. Kanuni na utaratibu wa utoaji. Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

Naam. Karibu tena. Twalichambua fungu la neno. 2 Wakorintho 8:16-9:5. Kanuni za utoaji wa fedha kanisani. Nasom Fungu hili la neno. 2 Wakorintho 8:16-9:5.

16 Tangu sasa hatumtazami mtu ye yote namna ya kibinadamu, ingawaje hapo mwanzo tulimtazama Kristo kwa namna ya kibinadamu. Hatumtazami hivyo tena.

17 Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, mapya yamekuja.

18 Haya yote yanatoka kwa Mungu, ambaye kwa njia ya Yesu Kristo ametupatanisha na mwenyewe, na akatupa huduma ya upatanisho.

19 Ndani ya Kristo Mungu aliupatanisha ulimwengu na yeye mwe nyewe, asiwahesabie watu dhambi zao. Naye ametukabidhi ujumbe huu wa upatanisho.

20 Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, Mungu anatutumia sisi kuwasihi ninyi. Na sisi tunawasihi ninyi kwa niaba ya Kristo: mpatanishwe na Mungu.

21 Mungu alimfanya yeye ambaye hakujua dhambi, awe dhambi kwa ajili yetu ili ndani yake tupate kuwa haki ya Mungu.

6 Kama wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure. 2 Kwa maana Mungu anasema: “Wakati ufaao niliku sikiliza, na siku ya wokovu nilikusaidia. Tazameni, huu ndio wakati ufaao; leo ndio siku ya wokovu.”

Katika fungu hili la neno twapata kanuni kadhaa kuhusu utoaji wa fedha na mali kanisani. Kwanza kabisa twaona ya kwamba katika mstari wa 16-18, Paulo anawataja tu ndugu wawili, Tito na ndugu mwingine, jina lake halikutajwa. Baadhi ya wasomi wamefikiria kuwa huyo ndugu mwingine alikuwa Luka ama Tofima. Pia palikuwa na ndugu mwingine ambaye jina lake limebanwa, walikuwa ndugu watatu Wakristo waaminifu na ndio walipewa kazi ya kuwaangalia na kusimamia utumikaji wa utoaji wa zile pesa.

Wanaosimamia hazina za kanisa zetu wanapaswa kuwa Wakristo waaminifu. Wakristo waaminifu ambao hawatakubali kutumia pesa za kanisa vibaya hata wakishawishiwa. Tito na ndugu wawili walikuwa waaminifu katika huduma hiyo ya upokeaji na utoaji wa pesa za kanisa

Ukweli wa pili wapatikana katika sura ya 8:19-22. Paulo aonyesha ya kwamba alipopeleka kile kipawa cha pesa kule Yerusalemu, ilibidi asafiri na ndugu waaminifu, wasije wakalaumiwa na mtu yeyote.

Nasoma tena maneno ya mstari wa 20.

Na tukifanya hivyo tutakuwa vyombo vya kueneza injili kwa watu wengine. Tusiwe watu wa kulaumiwa kama anavyosema Paulo katika mstari wan ne: 2 Wakorintho 9:4.

Mambo ya pesa ni mazuri lakini yanahitaji uaminifu sana katika kila jambo. Haijalishi kiasi cha fedha ile, uaminifu lazima uzingatiwe.