Junsi Ya Kumpendeza Mungu

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Junsi Ya Kumpendeza Mungu
/
Warumi 8:5-13

Hujambo leo twalichambua fungu la neno la mungu, Warumi 8:5-13 jinsi ya kumpendeza mung. Jina langu ni david mungai, wimbo alafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena tujifunze neno la mungu, waraka wa Paulo kwa warumi 8:5-13. Kila mtu aliye na mungu ndani yake hutafuta njia za kumpendeza mungu lakini tamaa za kimwili na dunia na kiburi cha uzima huwa changamoto kweli.

Nasoma sasa waraka wa Paulo kwa warumi 8:5-13

5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.

6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.

7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.

8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.

11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

12 Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili,

13 kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.

Hapa twaona Paulo akielezea namna tunavyoweza kumpendeza mungu

Jambop la kwanza ni kupeleleza namna akili zetu zafaya kazi neno la mungu limeonyesha wzi kuwa wale wanaozingatia ya kimwili akili zao kufuatilia ya kimwili na ni adui kwake mungu. Ya kimwili hayawezi kumpendeza mungu Akili za kimwili hujitukuza mwenyewe nafsi yake mwenyewe hujawa kiburi na neno la sema

Mungu huwapinga wenye kiburi lakini huwapa wanyenyekevu neema

Twampendeza mungu tunapokuwa wanyenyekevu. Mungu alimpinga na kumfukuza shetani na malaika wake waasi kwa sababu ya kiburi, shetani alijaribu kuabudiwa kama mungu unyenyekevu ndiyo njia ya kumwendea mungu

Jambo la pili tukimruhusu roho mtakatifu kutawala tutampendeza kristo aliye ndani yetu

9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

Kunao upya wa Maisha katika yesu kristo aliyefufuliwana mwenyezi mungu kutoka kwa wafu. Ndipo Paulo akatushauri