Injili Kwa Watu Wote

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Injili Kwa Watu Wote
Loading
/
Warumi 1:14-17

Hujambo msikilizaji, jina langu ni David Mungai na ni furaha yangu kukuletea somo kutoka waraka wa Paulo kwa warumi 1:14-17, Injili ni yako. Sikiza wimbo alafu tuendelee.

Wimbo

Naam karibu tena tujifunze neon. Warumi 1:14-17, injili kwa wote.

Kuna dini mbalimbali nao waumini wa dini hizo ni tofauti, lakini ukristo siyo dini tu bali ni ya watu wote maana yesu aliwakaribisha wote wayahudi na watiw a mataifa yote duniani. Tunao mataifa 195 duniani na wote wamealikwa na hivi ndivyo Paulo awakumbusha waumini wa kanisa lililokuwa roma. Nasoma sasa kutoka Warumi 1:14-17

14 Ninalo jukumu kwa watu wote, waliostaarabika na wasiostaarabika, wenye elimu na wasio na elimu.

15 Ndiyo maana ninatamani pia kuihubiri Habari Njema kwenu ninyi mlioko huko Roma.

16 Sioni aibu kutangaza Habari Njema; yenyewe ni nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na wasio Wayahudi pia.

17 Kwa maana Habari Njema inaonyesha wazi jinsi Mungu anavyowakubali watu kuwa waadilifu; jambo hili hufanyika kwa imani, tangu mwanzo mpaka mwisho. Kama ilivyoandikwa: “Mwadilifu kwa imani ataishi.”

Kutoka kwa fungu hili la neno, Paulo aliwaonyesha

Injili kwa watu wote

Kuhubiri injili ni lazima

Tuanze na ukweli wa kwanza injili ya wokovu ni kwa wote . kwanza kabisa Paulo asihi kwamba ni kama mtu aliyekuwa na deni lake yesu kwa sababu Paulo alipokuwa katika harakati za kuwatesa waliomcha mungu, yesu mwenyewe kwa upendo na uweza mwingi alimtokea Paulo na akamuuliza mbona wanitesa? Aliangushawa chini na Paulo akamlilia yesu, naye yesu kwa upendo ,wingi akamwokoa na kumtumia awapelekee waiowayahudi injili ya wokovu kwa hiyo sasa Paulo akaandika warumi ajiona kama anamdai yesu makuu, sikiliza kwa makini maneno ya mstari wa 14:

14 Ninalo jukumu kwa watu wote, waliostaarabika na wasiostaarabika, wenye elimu na wasio na elimu.

15 Ndiyo maana ninatamani pia kuihubiri Habari Njema kwenu ninyi mlioko huko Roma.

Deni humwasha mtu mno na ndivyo alivyokuwa Paulo katka kuhubiri injili ya wokovu katika kristo Yesu.

Kuhubiri injili ni lazima na ni ,zigo kwa mtu binafsi

Nasoma maneno ya mstari wa 16 na 17

16 Sioni aibu kutangaza Habari Njema; yenyewe ni nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na wasio Wayahudi pia.

17 Kwa maana Habari Njema inaonyesha wazi jinsi Mungu anavyowakubali watu kuwa waadilifu; jambo hili hufanyika kwa imani, tangu mwanzo mpaka mwisho. Kama ilivyoandikwa: “Mwadilifu kwa imani ataishi.”

Nahubiri injili kwa sababu ni uweza wa mungu uletao wokovu uzima wa milele kwa kila mtu anayetubu na kuungama dhambi zao na kumpokea yesu moyoni, myahudi na muyunani pia injili ya wokovu katika jina la yesu ni kwa kila mmoja wetu duniani kote.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!