Huwezi Kuhepuka

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Huwezi Kuhepuka
Loading
/
Warumi 2:1-22

Hujambo na karibu tujifunze neneo la Mungu pamoja. Leo twalichambua fungu la neneo kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 2:1-11 Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

Naam karibu tena. Twalichambua fungu la neon la Mungu kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 2:1-12 ‘Huwezi Kuepuka’

Sidhani kuna nchi duniani hii ambayo kweli haina jela mahali ambapo wahalifu huwekwa. Wachache huhepa lakini kwa ugumu, lakini huhepa kutoka kwa sharia za Mungu ni vigumu, na ukweli ni kwamba hukumu ya Mungu ipo.

Nasoma sasa fungu hili la neon la mungu. Waraka wa Pauko kwa Warumi 2:1-12

“Basi, rafiki, kama unawahukumu wengine, huwezi kamwe kujitetea, hata kama wewe ni nani. Kwa maana, kwa kuwahukumu wengine, unajilaani wewe mwenyewe kwa vile nawe unayafanya mambo yaleyale unayohukumu.

2 Tunajua kwamba hukumu ya Mungu kwa wale wanaofanya mambo kama hayo ni hukumu ya haki.

3 Lakini wewe rafiki unayewahukumu wale wanaofanya mambo kama hayo hali wewe pia unayafanya, je unadhani utaiepa hukumu ya Mungu?

4 Au labda unaudharau wema wake mkuu, uvumilivu wake na saburi yake, bila kutambua kwamba wema wake huo una shabaha ya kukuongoza upate kutubu?

5 Lakini unao ugumu na ukaidi wa moyo, na hivyo unajirundikia adhabu kwa siku ile ya ghadhabu wakati hukumu ya haki ya Mungu itakapodhihirishwa.

6 Siku hiyo Mungu atamlipa kila mmoja kufuatana na matendo yake.

7 Wale wanaozingatia kutenda mema, kutafuta utukufu na heshima ya Mungu na kutokufa, watapata uhai wa milele.

8 Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

9 Mateso na maumivu yatampata binadamu yeyote atendaye uovu. Yatawapata Wayahudi kwanza na watu wa mataifa mengine pia.

10 Lakini Mungu atawapa utukufu, heshima na amani wale wanaotenda mema; Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia.

11 Maana Mungu hambagui mtu yeyote.

12 Wale wanaotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria.

Neno linasema na kuonyesha wazi ya kwamba hakuna hata mmoja awezaye kuepa au kuepuka hukumu yake Mungu, kwa sababu tatu:
-Hukumu ya Mungu ni kweli
-Hukumu ya Mungu ni ya haki
-Hukumu ya Mungu ni kwa watu wote.

Hukumu ya Mungu ni ya kweli , kulingana na maneneo ya mstari wan ne wa fungu hili mstari wa nne.

“Au labda unaudharau wema wake mkuu, uvumilivu wake na saburi yake, bila kutambua kwamba wema wake huo una shabaha ya kukuongoza upate kutubu?”

Utahukumiwa kwa kweli hata wewe umeuona wema wa Mungu. Labda umesahau ya kuwa ni Mungu amekuruhusu kuishi, amekupa muda upate kutubu. Ukipuuza basi hukumu ya Mungu ya kweli ipo.

Mst 5. Lakini unao ugumu na ukaidi wa moyo, na hivyo unajirundikia adhabu kwa siku ile ya ghadhabu wakati hukumu ya haki ya Mungu itakapodhihirishwa.

Maneno hayo yanaonyesha na kutuarifu kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki. Wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu. Lakini yeyote aliye na saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoharibika watapewa uzima wa milele; na wale wenye hitima wasiotii kweli, bal wakubali dhuluma watapata hasira na ghadhabu.

Kila mtu atapata haki yake- Mst 10

“Lakini Mungu atawapa utukufu, heshima na amani wale wanaotenda mema; Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia.”

Kwa nini?

Mst 11. “Maana Mungu hambagui mtu yeyote.”

Hakuna atakayeepuka au kuhepa hukumu yake Mungu. Lakini habai njema ni kwamba yale ambayo hatuwezi kukamilisha kwa matendo yetu twaweza kwa imani an kumwamini aliyelipa hukumu pale msalabani; kwa niaba na kwa ajili yetu sisi wenyewe dhambi ile kwa kumwamini tuwe wavumilivu wa mji wa mbinguni.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!