Hukumu Ni Lazima Ipo

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Hukumu Ni Lazima Ipo
Loading
/
Mathayo 23:29-36

Hujambo! Hiki ni kipindi cha matumaini. Leo twajifunza kutoka injili ya mathayo 23:29-36. “Hukumu ni LAZIMA.” Jina langu ni David Mungai.

Jamii karibu zote duniani huwahukumu wakosaji. Wazee wa mtaa wajua hutoa hukumu kwa makossa tunaotenda. Na hukumu ni muhimu, ili tuwe na Amani. Yesu alifundisha kuweko kwa hukumu aliposema na waandishi na mafarisayo katika Injili ya Mathayo 23:29-36.

Ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii na kuyapamba maziara ya wenye haki. Na kusema kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungarishirikiana nao katika damu ya manabii. Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. Enyi nyoka, wana wa majoka mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji.

Hivyo ijie juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi tangu damu ya Habili, yule mwenye haki hata damu ya Zakaria bin Baraka mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. Amin, nawaambieni, mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.

Msikilizaji kunazo hali na mambo yanayotuzingira na kweli yahitaji kukemewa na kuhukumiwa. Katika fungu hili la neno la mungu, twaona ya kwamba waandishi na mafarisayo walikuwa wanafiki na waliyapa kipao mbele yale yaliyopita na kuukana uhusiano wao na baba zao.

Walisema “Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii” Walijaribu kuliondolea lawama la vile baba zao waliwaua na kuwatesa manabii, watu wa mungu, lakini Yesu awaambia kwamba wao ni kama baba zao, kwa sababu karibuni matanitesa mimi na wafuasi wangu. Hamna tofauti kati yenu na baba zenu. Ninyi wanafiki mwakiri yasiyo kweli, yanayohitaji hukumu kali. Kama tunavyosema maneno ya mstari wa 32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. Enyi nyoka wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehamanu? Kwa sababu hiyo, angalieni mimi natuma kwenu manabii, na wenye hekima na waandishi na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulubisha na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji. Hiyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi. Tangu damu ya Habili yule mwenye haki hata damu ya Zakaria bin barakia mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. Mambo hayo yote yalilundikana hivyo kwa sababu walikataa huruma zake mungu. Hilo ni jambo la kuogofya kwa sababu kama wangaliyashika ya manabii, wangalijiondolea hukumu ya mungu, Lakini walikataa wakamwasi mungu. Waliwaua watumwa na manabii wa mungu. Kwa hiyo wakaipata hukumu ya maradufu. Wanafiki waliishi na hukumu yao. Wanafiki wamejihukumu wenyewe mioyoni mwao. Hali kadhalika, mtu akiasi na kukataa magizo yake mungu bila shaka atahukumiwa na itakuwa vibaya ukijihukumu, nafasi ipo. Mrudie Bwana Yesu Kristo ni mwingi wa rehema na huruma.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!