Hukumu Itatolewaje

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Hukumu Itatolewaje
Loading
/
Warumi 2:12-16

Hujambo msikilizaji wangu mahala popote ulipo. Jina langu ni DavidMungai. Leo twalitazama fungu la neon kutoka Waraka wa Paulo kwa Warumi 2:12-16 Hukumu ya Mungu- Itatolewaje? Karibu wimbo halafu tuendelee

WIMBO

Naam. Karibu tena, tulichambue neno. Waraka wa Paulo kwa Warumi 2:12-16 Hakuna taifa wala kabila duniani ambalo kweli halina desturi n ahata sharia za kuwasaidia wananchi kuishi kwa Amani.

Mungu pia kwa neema yake na upendo wake ametuonyesha wazi, sharia zake kwa lugha rahisis kueleweka. Mungu kweli amejidhihirisha kwetu- Nani mwingine angeumba yale tunayoona na macho yetu, na nani mwingine ana uweza wa kuumba binadamu kwa njia kuogofya na kutisha.

Lakini swali ni hili. Katika hukumu yake Mungu- wetu, anatumia mbinu gani kutoa hukumu yake.

Nasoma neno kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 2:12-16

12 Wale wanaotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria.

13 Maana sio wanaosikia sheria ndio walio waadilifu mbele ya Mungu, ila wenye kuitii sheria ndio watakaokubaliwa kuwa waadilifu.

14 Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria.

15 Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea.

16 Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.

Wau wote watahukumiwa kulingana na sharia za Mungu.

(1) Huku itatolewa kulingana na Torati- Amri kumi zilitolewa ka mkono ya Musa. Na amri kumi zikapigwa katika agano jipya.

Mathayo 22:37-40 ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote’.

38 Hii ndiyo amri kuu na ya kwanza.

39 Ya pili inafanana na hiyo: ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe’.

40 Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili.”

Neno linaendelea kusema…

Mst 12 wa Warumi 2

1 ‘Wale wanaotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na
wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria.’ Je wampenda Mungu kiasi agni? Na adui yako?

2 Pamoja na hayo, Mungu atatumia maumbile yake kuhukumu. Mst 14
“Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria. Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea. Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo.”

Waraka wa Tito 2:11-14

Maana neema ya Mungu imedhihirishwa kwa ajili ya wokovu wa watu wote.

12 Neema hiyo yatufunza kuachana na uovu wote na tamaa za kidunia; tuwe na kiasi, tuishi maisha adili na ya kumcha Mungu katika ulimwengu huu wa sasa,

13 tukiwa tunangojea siku ile ya heri tunayoitumainia, wakati utakapotokea utukufu wa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

14 Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe kutoka katika uovu wote na kutufanya watu safi walio wake yeye mwenyewe, watu walio na hamu ya kutenda mema. Hiyo ni sharia ya Injili yote ya Siri yatahukumiwa kulingana na Injili ya bwaba wetu Yesu Kristo. Sote tuko chini ya hayo. Mungu atayahukumu hata yake ya siri, kulingana na sharia ya Injili. Tubu dhambi zetu na kumkiri Kristo kuwa Mwokozi waondolewe hukumu ya kutupewa katika bahari ya moto uwakao na kiberiti na kujitawalia ahadi ya uzima wa milele pamoja na Yesu.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!