Hofu Ya Tabia Za Kimwili

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Hofu Ya Tabia Za Kimwili
/
I Wakorintho 3:1-9

Msikilizaji hujambo. Natumai u buheri wa afya na kwamba u tayari kujifunza neno la Mungu pamoja nami.
Twalichambua neno la Mungu kutoka 1 wakr 3:1-9 ‘Hofu ya tabia za kimwili’

Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam, karibu tena tujifunze Neno la Mungu. 1 wakr 3:1-9.

Katika sharika zetu tunao waumini ambao wanabubujika katika matendo mema, kama matunda ya kujazwa na Roho na Zaidi wao walipenda Neno. Kunao wengine ambao tangu wamwamini Yesu wako pale, matendo yao hayana tofauti na yale waliofanya kabla ya kuokolewa. Ni wakristo wanaongozwa na tamaa za kimwili. Hawalipenda neno walihudhuria ibada ili na kuondoka. Pole pole watabalika bora walipende neno.

Lakini ni hatari na ni hofu kuu kuongozwa na tamaa za kimwili. Twahitaji kukua kiroho. Ni muhimu!

Hatupaswi kukaa tu, bila chakula cha kiroho. Si vizuri kubaki tu pale watoto wa kiroho. Nasoma fungu hili la neno 1 wakr 3:1-9

1 lakini ndugu zangu mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo ’

2 naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula, kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi

3 kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana ikiwa kwenu kuna husuda (jealousy)na fitina je!si watu wa tabia ya mwilini ninyi, sasa mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?

4 maana hapo mtu mmoja asemapo, mimi ni wa Paulo na mwingine mimi ni wa Apollo, je, ninyi si wanadamu?

5 Basi Apollo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini na kila mtu kama Bwana alivyompa

6 Mimi nilipanda, Apolo akatia maji, bali mwenye kukuza ni Mungu

7 Hivyo apandaye si kitu, wala atiaye maji bvali Mungu akuzaye

8 Basi yeye apandaye, nay eye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe

9 maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu, ninyi ni shamba la Mungu, na jingo la Mungu

Kutoka kwa neno hili la Mungu, twaona ya kwamba wakristo wa kanisa la korintho, watajwa na Paulo kuwa watoto katika mambo ya kiroho, kwa sababbu kwao kulikuwa na husuda na fitina. Msikilizaji, hebu fikiria kwa muda, ni kanisa gani au shirika gani ambalo husuda na fitina havyonekani wazi, haswa wakati wa kujagua viongozi?

Neno la Mungu limetuita ‘watu wenye tabia ya mwilini’, nini maana yake?

Neno la kigiriki ‘sarkinos’ latoa maana ‘enye tabia ya kimwili’ ikiimaanisha kwamba mwenye kuongozwa na tabia za kimwilini, kwa mfano, husuda na fitina, ni wanyonge na wadhaifu kiroho, watoto wachanga ndani ya Kristo, hawajakuzwa kwa neno, hawawezi na kweli za ndani kutoka nenoni mwake Mungu, matokeo yake – husuda na fitina.

Pamoja na hayo, katika mstari wa tatu twapata maneno haya, kwa maana hata sasa…..yaani wakristo wa kanisa la korintho hawakuwa na sababu ya kuishi katika hali ya watoto wachanga wa kiroho, na miaka mingi imepitatangu waokoke, na walienenda kwa jinsi ya kibinadamu. Na wakristo kama hao, hawa tofauti kimatendo na wale ambao bado hawajampokea Kristo kuwa mwokozi na mkombozi ili kukua, kiroho, sharti na lazima ukomboe wakati, panga masaa yako vile unakula chakula cha mwili, uwe na wasaa wa kukula chakula cha kiroho- kulisoma neno, kulitafakari na kujitwalia ahadi na kweli za neno, maishani mwako.

Jambo la tatu ni kuwa na umoja na wakristo wengine, na kushirikiana bila mashindano, ukweli huu umedhibitishwa na maneno ya mstariwa 8
‘basi yeye apandaye nay eye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe’

Tufanye kazi ya Mungu kwa ushirika na umoja na kwa utukufu wake Mungu. Mungu atusaidie tuwache kupuuza wito wake. Hofu na tabia za kimwili, huua ujasiri wa kukua kiroho, huwagawanya wakristo, hupuuza mapenzi ya Mungu maishani.

Twaweza kupata ukombozi kwa kupalilia ushirika wetu na Yesu Kristo bwana wetu. Amina