Heshima Kwa Viongozi

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Heshima Kwa Viongozi
Loading
/
I Wakorintho 4:10-15

Msikilizaji wangu mpendwa, u buheri wa afya, na karibu tujifunze Nneo pamoja. 1 Wakorintho 4:10-15, “Heshima kwa viongozi” Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO


Naam, karibu na tujifunze Neno pamoja. Katika Neno la Mungu, 1 Wakorintho 4:2 lasema, “Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.”

Mawakili na mabalozi wa Bwana wetu Yesu Kristo, wapaswa kuonekana waaminifu. Hata nyakati zingine tutadhihakiwa na kudharauliwa kama wapumbavu. Hebu na tusome 1 Wakor 4:10-15. Kumbuka twafikiria namna tunavyoweza kuwaheshimu viongozi wetu. Nasoma 1 Wakor 4:10-15

10 Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo, sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu, ninyi mna utukufu lakini sisi hatupati heshima.

11 Hata saa hii ya sasa tuna njaa na kiu , tu uchi, twapiga ngumi, tena hakuna makao.

12 Kisha twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa, twabariki, tukiudhiwa twastahimili.

13 tukisingiziwa twasihi, tumefanywa kama takataka za dunia, na tama ya vitu vyote hata sasa.

14 Siyaandiki hayo ili kuwatayarisha bali kuwaonya kama watoto niwapendao.

15 Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu, kwa njia ya Injili.

Paulo, awaarifu wakristo wa Korintho kwamba wao, yaani Apolo na Paulo mwenyewe, licha ya kuwa na elimu haswa katika Neno la Mungu, wamekuwa wapumbavu hata wakidhihakiwa na kutukanwa kwa sababu ya imani yao, wanayo nguvu maana hawana uti wa mgongo wa dunia hii, bali kwa Kristo.

Twanyenyekea hata tunapozingatia haki zetu katika kueneza injili na kusimamia imani yao. Paulo, awaita Wakristo wa Korintho, waheshimiwa. Hawajigambi wala kujivuna bali wanyenyekea na kuliinua jina la Bwana Yesu Kristo maishani mwao na katika huduma.

Hali hii ya akina Paulo na Apollo, yanikumbusha maneno ya Yesu mwenyewe katika Injili ya Mathayo 5:11,12 na 44.

11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.

12 Furahini, na kushangiliga, kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliyokuwa kabla yenu.

44 Mmesikia kwamba imenenwa, umpende jirani yako na umchukie adui yako; walakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu waombeeni wanaowaudhi…”

Haya basi yaonyesha kinyume cha vile walimwengu hutarajia. Manabii pia waliyapitia hayo. Mwandishi wa waraka kwa Waebrania atukumbusha: Waebrania 11:37

“Walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno(Yeremia na Isaya) walijaribiwa, waliuawa kwa upanga, walizunguka zunguka na ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi walikuwa wahitaji wakiteswa, wakitendewa mabaya (38 watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizungu-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.

39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi,

40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.

Hayo yote kwa ajili ya Injili, yenye utajiri wa mbinguni. Nini sababu au makusudi ya kuandikwa kwa maneno hayo:

Mst 14-15 1 Wakor 4:14-15

14 Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha bali kuwaonya kama watoto niwapendao.

15 Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo walakini hamna baba wengi

Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili. Basi mimi nawasihi mnifuate mimi.

Ni ushuhuda uliokuwa wazi kwa kila mtu, nah ii ndiyo njia ya kujitwalia heshima. Ushuhuda unaolingana na matendo ya mtu, na kila mtu asikia na hata kuona.

Je, ushuhuda wako wa maneno na vitendo. Je, zaenda sambamba?

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!