Hekima Ya Mwanadamu Si Kitu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Hekima Ya Mwanadamu Si Kitu
Loading
/
I Wakorintho 2:6-10

Hujambo na karibu tujifunze Neno pamoja. Twalichambua fungu la Neno la Mungu kutoka 1 Wakor. 2:6-10. “ HEKIMA YA MWANADAMU SI KITU”. Jina langu ni David Mungai. Wimbo halafu tuendelee.

WIMBO

Naam. Karibu tena tujifunze Neno pamoja. “ HEKIMA YA MWANADAMU SI KITU”. Hautoshelezi, kama tunavyosoma kutoka 1 Wakorintho. 2:6-10.

Akili za mwanadamu hushangaza. Zaweza kufanya mengi na makuuu. Lakini Mungu asipoturuhusu hafui dafu. Nyakati nyingi, uelefu na hekima zetu, hututayarisha. Hutuangusha vibaya. Hekima, afadhali kulika ujuzi na uelefu pasipo uwepo wa mwenyezi Mungu.

Katika nchi fulani kulikuweko na kundi la watu waliodhani na kufikiri kuwa maji ya visima huwa na mapepo, ambao husababisha maradhi na magonjwa. Ilichukua muda kiasi kuwaelemisha lile kundi la wananchi, kwamba kuchemsha maji huua viini vinavyosababisha maradhi.

Akili za binadamu bila kuwezeshwa na mwenyezi Mungu haziwezi. Nasema sasa kutoka 1 Wakor. 2:6-10.

6 Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu, ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika,

7 bali twanena hekima ya Mungu katika siri ile hekima iliyofichwa ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu

8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulubisha. Bwana wa utukufu,

9 lakini kama ilivyoandikwa: mambo ambayo jicho, halikuyaona wala sikio halikuyasikia (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu). Mambo ambayo mungu aliwaandalia wampendao.

10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. “
Kwa nini hekima ya mwanadamu, si kitu. Paulo atoa jibu katika mstari wa 6.

Hekima ya dunia hii hubatilika ,yaani ni bure- ni zilo- hekima ya dunia haipati jibu au suluhisho la kudumu.

“Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu, ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanayoitawala dunia hii wanaobadilika.”

Hekima ya dunia hii haidumu. Walawala hao huondoka, wengine hushika usukanii na wao baadaye huondoka, na wengine huja na uvumbuzi mpya.

Sababu ya pili. Hekima ya dunia imefichwa. Maneno ya mstari wa saba na wa nane:
“bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima ilivyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu, (8) ambayo wenye kuitawala dunia hii hawajui hata mmoja; maana kama wangaliijua wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu.”

Paulo hakupenda Imani ya Wakristo wa Korintho kutawaliwa na mabishano, waliofikiria kuwa ni wajuaje kuliko Mungu, bali aliwaombea watawaliwe na nguvu kutoka kwake mwenyezi Mungu.

Wakorintho walikuwa kama lile kundi la wakuu wa dini ya Kiyahudi. Sanhedrin Na Petero, alipopata nafasi ya kuwahudumia, aliwaambia maneno haya: (Matendo 3:12-17)

12 Hata Petro alipoyaona haya, akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu. Sisi au kwa utauwa wetu sisi?

13 Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.

14 Bali ninyi mlimkana yule mtakatifu, yule mwenye haki, mkatakampewe mwuaji.

15 mkamwua yule mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu, na sisi tu mashahidi wake.”

Wote wawili, Petro na Paulo, wamekubaliana kwamba, hekima ya kibinadamu, hawezi kwa sababu nia zao zahitilatiana. Lazima tuamue, kwa uyasiri, kuyazingatia ya Imani yetu katika Kristo bila kuruhusu hekima ya binadamu, ya kimwili na ya dunia kututatiza juhudi zetu za kiroho.

Sababu ya tatu: Nasoma mstari wa 9-10

“lakini kama iliyoandikwa (Isaya 64:4) mambo ambayo jicho halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.”

Katika kifupi Paulo ataka tujue ya kwamba, tukizingatia sababu zetu binafsi, hatutaweza kujua yale Mungu ametuwekea sisi tunaompenda. Na hii ndiyo sababu Mungu ametupalia Bibilia. Neno lake la hekima yote.

Duniani tunayo mambo, na sauti ni nyingi za tuita, lakini naomba tulizingatie Neno la Mungu, na kujifunza kujiuliza.

Katika mambo hayo yote, Mungu amesema nini katika Neno lake. Tulisome Neno na kulitafakari, mioyoni mwetu. Neno la Mungu hutuongoza kila jambo, tukisaidiwa maagizo ya Neno, na utafsiri wake Roho Mtakatifu. Hiyo ndiyo hekima inayoleta faida maishani yetu ya Kikristo

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!