Hali Ya Injili

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Hali Ya Injili
Loading
/
Warumi 16:24-27

Natumai u buheri wa afya msikilizaji wangu. Naitwa David Mungai na ni furaha yangu kukuletea MATUMAINI tujifunze neno pamoja. Warumi 16:24-27 HALI YA INJILI. Wimbo halafu tuendelee.

Wimbo

Naam. Karibu tena tujifunze Neno pamoja- HALI YA INJILI kama linavyoeleza Neno kutoka waraka wa Paulo kwa Warumi 16:24-27

Waumini wa zamani walivyomfuata Yesu Kristo waliitwa wakristo. Na msingi wa Imani ya Kikristo, ni Kristo Mwenyewe.

Ni muhimu imani yetu katika Kristo iwekwe muhuri kwa maneno na matendo yetu. Imani yetu katika Kristo ndiyo njia ya kipekee ya kuleta amani kati yetu na Mungu Baba. Hebu tumsikize Paulo akieleza Hali ya Injili!

Warumi 16:24-27

24 ( Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amina. )

25 Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na Injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele.

26 Ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.

27 Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina. HALI YA INJILI – Ni huduma ya kumhubiri Yesu Kristo.

Yaani injili ni mahubiri yanayomhusu Yesu Kristo, na Habari njema. Kwa wanaomwamini, lakini wanaokataa kupokea habari hii njema ya wokovu, basi hakutakuwa na cha ziada ila ni kutupwa tu kuzimu na bahari ya moto.

Ni siri inayofumbuliwa katika Kristo yesu.

Ni fumbo ambalo hufumbuliwa kwa kutubu dhambi na kumpokea Yesu moyoni.

Injili ya Bwana Yesu Kristo, ni DHIHIRISHO. Injili imewekwa wazi kwa yeyote anayemwamini Yesu. Mstari wa 26 “ ikadhihirishwa wakati kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele waitii imani.

Injili Imedhihirishwa Kwetu kwamba ni habari njema tupate kumwamini Yesu Kristo, kusudi tuwe na amani ya moyoni tukimkabidhi mungu fadhaa zetu zote, maana ajishughulishe sana na mambo yetu. Injili hudhihirisha amani ya moyoni ili tuitii imani. Neno limesema hivyo.

Jambo la tatu ni amri kutoka kwa mwenyezi Mungu- Tumwamini Yesu Kristo.

Mstari wa 26 tena… “ Ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.”

Ni hatia na ni makosa kukaidi amri yake Mungu. Na hii injili ni kwa ajili ya mataifa yote.

Na tumeipokea, na twaipokea kwa kumwamini maana ndiye njia ya mbinguni.Hamna njia nyingine.

Yesu Mwenyewe alisema; “ Mimi Ndimi njia na kweli na uzima.” Usidanganywe, hamna njia nyingine.

Hatuwezi kunyamaza, lazima tuikiri imani yetu katika Kristo na kuitangaza.

Tumepewa uwezo wa kuamini na kuitangaza. Hatuwezi kukaa kimya mpaka Yesu arudi kulinyakua kanisa lake, na hata baada ya kanisa kunyakuliwa, kuhubiri kutaendelea hata wakati wa dhiki kuu, kunao wayahudi watauliwa na Mpinga Kristo, kwa sababu ya imani yao.

Katika mateso mengi wengi watamuamini Kristo. Wayahudi na hata watu wamataifa wataipokea injili ya wokovu kwa imani kwa sababu roho mtakatifu bado atawala kati yetu.

Hakuna ujumbe mwingine unaoshinda ujumbe wa injili ya wokovu katika Yesu. Imefunuliwa na tumepewa nguvu na uwezo wa kuihubiri na kuitangaza, duniani kote.

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!