Furaha Ya Kujitoa Kwake Mungu

hft swahili 2022
Hope for Today (Swahili)
Furaha Ya Kujitoa Kwake Mungu
Loading
/
Warumi 6:8-13

Hujambo na karibu. Jina langu ni David Mungai na leo twalitazama neno kutoka Warumi 6:8-13 furaha ya kujitoa kwake mungu. Karibu wibo alafu tuendelee

Wimbo

Naam karibu tena waraka wa Paulo kwa Warumi 6:8-13

Mungu alimuumba adamu akamweka bustani mwa edeni kusudi wae wakishirikiana ilikuwa muhimu, adamu awe na husiano mwema na yule aliyemuumba lakini dhambi ikaharibu uhusiano huo. Bado kunao baadhi wanaofikiria wanaweza kuishi pekeyao bila mungu Biblia yasema kwamba asemaye hivyo au kuwaza hivyo ni mpumbavi, mpumbavu husema Hakuna mungu, zaburi 14:1

Lakini wanao jitoa kwake mungu na kumkiri wanayo furaha tele na huishi Maisha makamilifu

Sasa nasoma kutoka waraka wa Paulo kwa warumi 6:8-13

8 Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;

9 tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.

10 Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.

11 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

12 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;

13 wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.

Mtume Paulo alitupatia hatua kadhaa zinazotuelekeza katika hali ya kujitoa kwake mwenyezi mungu

Hatua ya kwanza ni kujua ya kwamba tulikufa na kristo na kwamba katika kristo twaishi maneno ya mstari wa nane yaweka muhuri ukweli huu

8 Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;

Twajitawalia ukweli huo kwa Imani

Htu Y pili kujihesabuni kuwa wafu kutoka dhambi mstari wa 10-11

10 Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.

11 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

Huo ni ukweli wa ajabu kwamba tujihesabu kuwa wafu katika dhambi lakini sis bado tuna miili na hisia zinazotufanya dhambi. Mungu aujua unyonge wetu na ndiyo sababu ametuonysha njia ya kutubu na kuungama kila wakati na kuacha njia za dhambi. Tuichkia dhambi na tusikubali kujenga viota vichwani mwetu

Hatua ya tatu; acha kuti misukumo ya dhambi. Mstari wa 12

12 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;

13 wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.

Furaha tele ni yetu tunapolitii neno hili. Kumbuka tulikufa na kristo msalabani

Tujihesabu wafu kutoka dhambini

Tuache kutii tamaa na misukumo inayotuelekeza katika dhambi inayotuelekeza katika dhambi. Tu viumbe vyipya katika kristo

Receive Weekly Encouragement

Sign-up to get a sermon straight to your inbox on a weekly basis!