Ahadi Za Utoaji

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Ahadi Za Utoaji
/
II Wakorintho 9:6-15

Hujambo msikilizaji wangu mpenzi na karibu tujifunze neno pomoja. Jina langu ni david Mungai. Leo twalichambua neno la Mungu kutoka kitabu cha 2 Wakorintho 9:6-15, AHADI ZA UTOAJI’. KARIBU WIMBO HALAFU TUENDELEE

Naam, karibu tena tujifunze neno pamoja 2 Wakorintho 9:6-15. nasoma

6 Lakini nasema neno hili apandaye haba atavuna haba. Apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu

7 kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni wala si kwa lazima maana mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu

8 na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa mingi ili ninyi mkiwa na riziki za kila namna siku zote mpate kuzidi sana katika kila tendo jema

9 kama ilivyoandikwa ametapanya amewapa maskini haki yake yakaa milele

10 na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda na mkate uwe chakula atawapa mbegu za kupanda na kuzidisha naye atayaongeza mazao ya haki yenu

11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu

12 maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani ninyi apewazo mungu

13 kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo wanamtukuza mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri injili ya kristo na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote

14 nao wenyewe wakiomba dua kwa ajili yenu wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu

15 Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo

Kwenye maneno ya mstari wa 6 na 11 twapata ukweli kwamba apandacho mtu ndicho huvubna ukweli huu pia umetajwa katika kitabu cha mithali 11:24

Kuna atawanyaye lakini huongezewa Zaidi kuna azuiaye isivyo haki lakini hueleka uhitaji hebu sikiza maneno ya mstari wa nane tena

Na maana aweza kuwajaza kila neema kwa wingi ili ninyi mkiwa na riziki za kila namna siku zote mpate kuzidi sana katika kila tendo jema

Mungu humzidisha mtu Baraka mwenye matendo mema kwa yeyote atoaye kwa moyo mkunjufu mstari wa kumi

Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda na mkate uwe chakula atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha naye atayoongeza mazao ya haki yenu

Na hata katika AGANO LA KALE mambo yalikuwa vivyo hivyo. Nasoma hosea 10:12

Jipandieni katika haki vuneni kwa fadhili uchimbueni udongo wa mashamba yrnu kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta bwana hata atakapokuja na kuwanyeshea haki

Ukipenda kupata mavuno ya haki panda katika haki. Acha unyanyasaji na udanganyifu toa kwa moyo mkunjufu

Tukitoa kwa mioyo mikunjufu na kwa haki kipawa cha pesa kitaondoa shida na changamoto za wengi katika shirika na kutoa shukrani. Nasoma mstari wa 12

Maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyinyi apewazo Mungu

Kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri injili ya Kristo na kwa ajili ya ukarimu mliowashirikisha wao, na watu wote

14 nao wenyewe wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu

15 Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake tusichoweza kukisifu kama ipasavyo

Wakristo wa Yerusalemu walionea shauku wakristo wa korintho kwa upendo na ukarimu wao.

Waliowaombea na kumshukuru Mungu. Na hiyo ndiyo ahadi ya utoaji kwa ukarimu ukifanya hicyo watamtamani na hata kutilia maanani Imani yao katika Kristo bwana na mwokozi wetu. Mungu ndiye anayetuahidi hayo.