Kwanini

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Kwanini
/
Zaburi 22:1-11

Hujambo na karibu mpenzi msikilizaji. Natumai ubuheri wa afya na ni furaha yangu kukuletea kipindi hichi cha matumaini. Leo twalichambua neon la mungu kutoka kitabu cha Zaburi 22:1-11. Kabla ya hayo yote, wimbo alafu tuendelee.

Naam karibu tena kila wakati twauliza swali hili, kwa nini? Kwanini niyapitie haya? Na nyakati nyingi hatupati jibu kwa sabau kuona au kujua jibu tunahitaji lakini tukimwamini kwamba mungu akalia kiti chake cha enzi basi twaondoa wasiwasi maana mungu ajua maana daima mungu yupo na yuko pamoja nasi hivyo ndivyo asema. Nasoma sasa fungu la leo Zaburi 22:1-11

Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Mbona uko mbali sana kunisaidia, mbali na maneno ya kilio changu? Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu; napiga yowe usiku, lakini nafuu sipati. Hata hivyo, wewe ni mtakatifu; wewe watawala na kusifiwa na Waisraeli. Wazee wetu walikutegemea; walikutegemea, nawe ukawaokoa. Walikulilia wewe, wakaokolewa; walikutegemea, nao hawakuaibika. Lakini mimi ni mdudu tu, wala si mtu; nimepuuzwa na kudharauliwa na watu.

Wote wanionao hunidhihaki; hunifyonya na kutikisa vichwa vyao. Husema: “Alimtegemea Mwenyezi-Mungu, basi, Mungu na amkomboe! Kama Mungu anapendezwa naye, basi, na amwokoe!” Lakini ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, uliniweka salama kifuani pa mama yangu.

Nimekutegemea tangu kuzaliwa kwangu. Tangu nilipozaliwa wewe umekuwa Mungu wangu. Usikae mbali nami, kwani taabu imekaribia; wala hakuna wa kunisaidia.

Zaburi hii ni moja yapo ya zaburi za mesiya yaani ina utabiri unaomhusu yesu hasa alipolia msalabani, mungu wangu munguwangu mbona umeniwacha

Ni kilio cha mtu aliyeachwa pekee. Labda wajihisi hivyo kwamba umeahwa pekeyako nakukumbusha ya kwamba hauko pekeyako, mungu baba yuko pamoja nawe kama wetu yesu kristo pale msalabani.

Mungu ayajua yote unayoyapitita hauko pekeyako.

Pamoja na hayo, mwandishi wa hii zaburi aonekana mpweke. wengine wamemkimbia na kwa hivyo akumbuka vile mungu aliwakomboa watu wake kutoka misri lakini katika zaburi hii watu wamcheka na kumdhihaki

Maneno hayo yatukumbusha Mathayo 27:43-44

Ametegemea mungu na amwokoe sasa kama anamtaka kwa maana alisema mimi ni mwana wa mungu pia wale wanyanganyi waliosulubiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.

Msikilizaji usihofu yesu kristo aliyeteswa msalabani pamoja nawe hauko pekeyako. Kristo yu pamoja nawe/nasi.

Yesu alipokuwa anakufa msalabani alilia kwa sauti kuu alisema eeh baba mkononi mwako naiweka roho yangu.

Mungu ayajua na kuyafahamu yote unayoyapitia. Heri umkabidhi yeye hayo yote kwa maombi naye atayafanya mapenzi yake masihani mwako

Bwana wetu yesu kristo aliyapitia hayo yote mshindi. Twasoma katika ahadi zake mungu tutakuwa washindi.