Kosa Kuhusu Ufufuo – Part 2

Hope for Today (Swahili)
Hope for Today (Swahili)
Kosa Kuhusu Ufufuo – Part 2
/
Mathayo 22:23-33

Hujambo na karibu. Hiki ni kipindi cha kujifunza neno la mungu. Kipindi cha matumaini. Kichwa cha somo letu ni “ Kosa kuhusu ufufuo” injili ya mathayo 22:23-33. Jina langu ni David Mungai.

Watu wengi sana duniani huamini ya kwmaba kunao uhai baada ya kifo. Baadhi ya watu huamini kwamba mtu aweza kufariki halafu afufuke akiwa mnyama. Hii ndiyo sababu wafalme wa baadhi za nchi wakifariki wao huzikwa makaburini mwao, pamoja na magari yao ya farasi na kadhalika. Ili waendapo wasisumbuke kukosa cha kusafiria. Wenyewe huamini kwamba roho atakuwa huru kutoka mwilini. Mazishi yalitayarishwa kwa urahisi sana.

Biblia hufunza ya kwamba tutafufuliwa na miili yetu ya utukufu, kama alivyofufuliwa Yesu Kristo. Nasoma sasa kutoka Injili ya Mathayo 22:23-33

“Siku ile masadukayo watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea wakamwuliza wakisema, Mwalimu, Musa alisema mtu akifa akiwa hana watoto ndugu yake na amwoe yule mkewe ili ampatie nduguye mzao. Basi kwetu kulikuwa a ndugu saba wa kwanza akaoa akafariki na kwa kuwa hana mzao akamwachia nduguye mke wake. Vivyo hivyo na wa pili naye na wa tatu, hata na wote saba. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. Basi katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika wale saba. Maana wote walikuwa naye. Yesu akajibu akawaambia mwapatea kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa mungu. Kwa maana katika kiyama hawapi wala hawaolewi bali huwa kama malaika mbinguni. Tena kwa habari ya kiyama ya watu hamjalisoma neno lililonenwa na mungu akisema, mimi ni mungu wa Ibrahimu na mungu wa Isaka na mungu wa Yakobo. Mungu si mungu wa wafu, bali wa walio hai. Na makutani waliposikia walishangaa kwa mafunzo yake.”

Katika mstari wa 23, masadukayo wametajwa na walikuwa watu wasioamini kwamba watu watafufuliwa, pia hawakuamini katika mambo ya toho. Waliamini kwamba mtu akifa hakuna uhai tena. Hata hivyo waliyajua machache kuhusu torati kumi za musa. Pia walijua ya kwamba mwanaume akifariki na hana watoto, ndugu yake aweza kumzalia watoto na yule mjane. Ndipo wakamwekea mtego ndugu wote wakifariki siku ya kiyama yule mke atakuwa wa nani?

Mara moja Yesu akawakosa akawaambia “Mwapotea, kwa kuwa hamyaji maandiko wala uweza wa mungu. Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi bali huwa kama malaika mbinguni. Msikilizaji, ikiwa tutakuwa kama malaika ukweli ni kwamba malaika hawana watoto. Mbinguni hatutaoa ala kuolewa.

Masadukayo walikosea wale hawakujua ufufuo utakuwa namna gani! Yesu alisema ya kwamba ufufuo umefunuliwa katika biblia, na kama wangalisoma biblia wangalijue na kuelewa ufufuo ni nini. Yesu alilinukulu agano la kale mungu aliposema na baba zetu wazamani.

Mst 32 “Mimi ni mungu wa Ibrahimu na mungu wa Isaka na mungu si mungu wa wafu bali wa walio hai” Kwa wakristo tutaishi hata baada ya kifo, ukweli ambao msingi wake ni mungu mwenyewe kwa sababu mungu wetu katika kristo aishi, milele na milele. Uzima wa milele tunao mara tu tunapomwamini Yesu Krsito. Mungu wetu ni wa walio hai kwa mungu hakuna kifo na twataraji kusihi naye kristo milele na milele.