II Wakorintho 11:1-5
Hujambo msikilizaji wangu mpenzi na karibu tujifunze neno pomoja. Jina langu ni david Mungai. Leo twalichambua neno la Mungu kutoka kitabu cha 2 Wakorintho 11:1-15 TABIA ZAKE PAULO. Wimbo halafu tuendelee.
Naam, karibu tena tujifunze neno pamoja 2 Wakorintho 11:1-15, nasoma
1 Laity ningechukuliana nami katika upumbavu wangu kidogo naam mchukuliane nami
2 maana nawaonea wivu wivu wa Mungu kwa kuwa naliwaposea mume mmoja ili nimletee Kristo bikira safi
3 lakini nachelea kama yule nyoka aliyemdanganyana hawa kwa hila yake asije akawaharibu fikira zenu mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo
4 maana yeye ajaye akiharibu Yesu mwingine amabye sisi hatukumhubiri au mkipokea roho myingine msiyoipokea au injili myingine msiyoikubali mnatenda vema kuvumiliana naye
5 maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu
6 lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena hii si hali yangu katika elimu ila katika kila neno tumedhihirishwa kwenu
7 je nalifanya dhambi kwa kunyeyekea ili nanyi mtukuzwe kwa sababu naliwahubiri injili ya Mungu bila ujira?
8 naliwanyanganya makanisa mali yao nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi
9 nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu . maana hao ndugu waliokuja kutoka makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu name katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo tena najilinda
10 kama vile ile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu hakuna mtu atakayenifumbua kinyawa katika kujisifu huku katika mipaka ya akaya
11 kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi . Mungu najua
12 lakini mifanyalo nitalifanya ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi ili kwamba katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi
13 Maana watu kama hao ni itume wa uongo walendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa kristo
14 Wala si ajabu . maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa huyu
15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki amabo mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao
Tabia zake Paulo kwa wakorintho zilikuwa mfano mwema kwa baba awapendao watoto wake aliona wivu kuwa wakorintho walikuwa wajigawa makundi makundi kundi la Apollo, kundi la Kefa, na la Paulo na linguine la Kristo
Kwa hiyo Paulo kama baba wa kiroho aliona wivu akatamani kuwarudi katika ushirika mmoja. Ni kama alivyo Mungu kwa aliona wivu sana kwa waisraeli walipotafuta nguvu n ahata misaada kutoka kwa
Mungu wengine kama tunavyosoma kutoka kitabu cha kutoa 34:14
Maana hutamwabudu Mungu mwingine kwa Bwana amabye jina lake ni mwenye wivu ni Mungu mwenye wivu
Katika desturi na utamaduni wa kiyahudi binti anapochumbiwa baba yake huhakikisha kwamba siku ya arusi atampeana binti yake akiwa bikira katika fungu hili la neno msichana aliyechumbiwa ni kanisa la Korintho kupitia huduma yake Paulo. Bwana harusi ni BWANA KRISTO. Siku ya harusi ni kurudi kwake Yesu Kristo kwa wakati huu kanisa limechambuliwa na YESU , lakini siku ya harusi itafika wakati wa kurudi kwake Yesu Paulo basi anahofia bwana arusi akija asikuje si bikira kwa hiyo aliwaomba wakorintho wakae na wadumishe Imani yao katika Kristo
2 wasiikumbatie injili ya aina nyingine ukiletwa na walimu wa wongo wanaojifanya wema kuliko Paulo mst 5-6 waalimu wa aina hii hutafuta sifa zao wenyewe na hata utajiri. Na ni wengi na tuko nao hata wa leo Paulo hakuwasumbua washiriki wa kanisa la korintho bali alifanya kazi kwa mikono yake kazi ya kutengeneza hema. Nasoma tena maneno ya mst 5-7
Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu (awadhihaki)
6 lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena hii si hali yangu katika elimu ile katika kila neno tumedhihirishwa kwenu
7 je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe kwa sababu naliwahubiri injili ya Mungu bila ujira
Paulo alikataa ujira kutoka kwa wakorintho akafanya kazi na mikono yale na kusaidiwa na makanisa ya makedonia na Akaya
Paulo awahimiza wakorintho wasimame imara katika Imani na kwa subira wangonjee siku ya kurudi kwake Yesu. Waache kudanganya na walimu wa dogo wanaotafuat sifa zao, tena kwa kiburi na mali Yesu alijima yote kwa ajili yetu sis pia tujinyime kama Paulo kwa ajili ya kanisa la Mungu